Afisa Habari, Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Temeke Lucia Renatus (kwanza kushoo) akitoa elimu kwa wananchi wa Mbande Kisewe, Dar es Salaam leo Oktoba 8, 2024 kuhusu matumizi ya jiko janja ambalo linatumia nishati safi ya umeme ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja ikiongozwa na kauli mbinu isemayo: Kutoa huduma bora juu na zaidi ya matarajio ya wateja na Shirika. (PICHA NA NOEL RUKANUGA).
Mhandisi Mkuu wa TANESCO Mkoa wa Temeke Mhandisi David Mhando akizungumza jambo wakati akitoa elimu kwa Wananchi wa Mbande Kisewe kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa matumizi ya Nishati Safi ya Umeme.
Afisa wa Huduma za Usalama TANESCO Mkoa wa Temeke Stephen Maganda akitoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuzingatia usalama wakati unatumia nishati safi ya umeme pamoja na umuhimu wa kulinda miundombinu ya TANESCO.
Maafisa Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Temeke wakitoa elimu kwa wananchi wa Mbande Kisewe.
Picha za matukio mbalimbali
NA NOEL RUKANUGA, DAR S SALAAM
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limewataka wananchi kutumia nishati safi ya umeme kwa ajili ya kupikia kupitia jiko janja ambalo linatumia gharama nafuu ya uniti moja ya umeme.
Akizungumza leo Oktoba 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akitoa elimu kwa Wananchi wa Mbande Kisewe kuhusu masuala mbalimbali ya TANESCO ikiwemo matumizi ya nishati safi ya umeme pamoja umuhimu wa kulinda miundombinu ya umme, Mhandisi Mkuu wa TANESCO Mkoa wa Temeke Mhandisi David Mhando, amesema kuwa wakati umefika kwa wateja kutumia nishati safi ya umeme ili kuondokana na nishati nyengine ambazo sio rafiki kwa ajili ya matumizi ya kupikia.
Mhandisi Mhando amesema kuwa umeme ni nishati rafiki kwa ajili ya kupikia, hivyo wananchi wanapaswa kuchangamikia fursa ya kutumia gharama nafuu kutumia jiko janja ambalo linatumia nishati ya umeme.
“Katika wiki hii ya huduma kwa mteja tunaweka mkazo wa matumizi mazuri ya umeme kwa kutumia nishati ya safi ambayo haitumii umeme mwingi” Mhandisi Mhando.
Amesema kuwa kuna faida kubwa ya kuwafikia wateja kwani wana hamasa kubwa ya kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutendaji ya TANESCO katika kuhakikisha kuwapata huduma bora.
“Baada ya wiki hii ya huduma kwa mteja tutaendelea kujipanga zaidi ili kuhakikisha huduma zetu zinaendelea kuwa bora na kukidhi matarajio ya wananchi” amesema Mhando.
Mhandisi Mhando amesema kuwa hali ya upatikanaji ya huduma ya umeme katika Mkoa wa Kitanesco Temeke inaendelea kuwa nzuri kwani kuna maboresho makubwa ya miundombinu ya umeme yanafanyika.
Amesema kuwa Mkoa wa Kitanesco Temeke kuna Wilaya ya Mbagala, Yombo, Kigamboni ambapo kuna miradi ya maboresho ya huduma ya umeme yanaendelea kutekelezwa.
Afisa Habari, Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Temeke Lucia Renatus, amesisitiza umuhimu wa matumizi ya nishai safi kutokana ni rafiki na nafuu.
Mhasibu Mkuu wa TANESCO Mkoa wa Temeke Lucy Mwaisemba, amesema kuwa wiki ya huduma kwa wateja ina manufaa makubwa kwa shirika kutokana inaongeza idadi ya wateja na mapato.
“Tumeweza kukutana na wateja na kutatua matatizo yao kwani awali walikuwa wanashindwa kutumia huduma ya umeme kutokana na changamoto ndogo ndogo na sasa mapato yetu yanakwenda kuongezeka” amesema Mwaisemba.
Nao Wateja wa TANESCO Mkoa wa Temeke akiwemo Fatuma Hamasi pamoja na Omary John wameridhishwa na huduma ya umeme inayopatikana kwa sasa ikiwemo kutumia nishati safi , huku wakitoa wito kwa Shirika hilo kuendelea kuwasiliza wateja wao jambo ambalo litaongeza ufanisi katika utendaji.
Katika wiki ya huduma kwa mteja wakazi ya Mbande Kisewe wamekuwa na mwitiko mzuri kwa kushiriki kwa idadi kubwa ya watu kwa ajili ya kupata elimu, kutoa maoni, ushauri pamoja na kupata ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya huduma.
Wananchi wa Mbande Kisewe wameonekana kufurahishwa na matumizi ya jiko janja ambalo linatumia nishati ya umeme, elimu iliyotolwa na TANESCO Mkoa wa Temeke ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja wakiongozwa na kauli mbinu isemayo: Kutoa huduma bora juu na zaidi ya matarajio ya wateja na Shirika.