Na Khadija Kalili Michuzi Tv
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amezindua kiatilifu hai cha kuangamiza wadudu dhurifu kwenye mazao kilichotambulika kama Thurisave-24
Uzinduzi huo umefanyika kwenye Kiwanda Cha Viuatilifu hai Cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kilicho chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo NDC kilichopo Wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Mhe. Bashe ametoa pongezi kwa Kiwanda hicho kwa kutengeneza viuatilifu rafiki kwa mazingira ambavyo vinaweza kuua wadudu ambao wamekuwa tishio katika sekta ya kilimo nchini.
Aidha Waziri Bashe amesisitiza umuhimu wa kutumia viuatilifu hivyo na kumuelekeza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa ajili ya viuatilifu zinatumika kununua bidhaa za TBPL na kuwafundisha wakulima jinsi ya kuvitumia ipasavyo.
Thurisave -24 inatumika kwenye mazao ya mahindi,pamba, tumbaku,viazi vitamu ,viazi mviringo, mihogo, kabeji, mbogamboga za majani, matunda na maharagwe.
Thutisave-24 ni kiuatilifu kisicho na madhara kinachoangamiza wadudu waharibifu wa mazao katika hatua ya viwavijeshi kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika bidhaa hii ina ufanisi wa hali ya juu katika udhibiti wa viwavi wa jamii ya Lepidoptera.
“Thurisave inahakikisha usalama wa ikolojia na afya za watumiaji kwakua haina sumu dhurifu na mazingira hivyo kutimiza malengo ya milenia”amesema Bashe.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Balozi wa Cuba nchini Mhe.Yordenis Vera, Meneja TPBL Mhandisi Rafael Moya ,Mwakilishi wa Bodi ya NDC Mhandisi ,
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge wafanyakazi wa NDC.