Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Amiri Mkalipa akizungumza katika mahafali hayo katika.shule ya mchepuo wa kiingireza ya Trust .St Patrick iliyopo mkoani Arusha.
Mtawala shule za Trust St.Patrick Schools, Bernadinnah Patrick akizugumza katika mahafali hayo.
Na.Happy Lazaro,Arusha .
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Amiri Mkalipa amewataka wanafunzi kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa lengo la kujifunza badala ya kuitumia vibaya jambo ambalo linaharibu maisha yao.
Ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akizungumza katika mahafali ya 16 ya kidato cha nne na mahafali ya 22 darasa la saba pamoja na darasa la awali katika shule za Trust .St Patrick iliyopo mkoani Arusha .
Amesema kuwa,kumekuwepo na tabia ya wazazi kuwapa watoto simu bila kufuatilia wanachokifanya kwenye mitandao hiyo jambo ambalo mwisho wa siku huwaaribu watoto hao kutokana na kujifunza vitu ambavyo havifai na kuwaharibia maisha ,hivyo kuwataka wazazi hao kuzungumza na watoto kuhusu matumizi sahihi ya mitandao.
“wazazi hakikisheni mnafuatilia kwa karibu matumizi ya simu yanayofanywa na watoto wenu kwani wengi wao hutumia mitandao hiyo tofauti jambo ambalo linachangia kuendelea kuwepo kwa mporomoko wa maadili.
Hata hivyo amewataka wazazi hao kuhakikisha wanawafundisha watoto wao kuhusu tamaduni mbalimbali ili watoto waendelee kuzienzi wakiwa tangu wadogo .
Kwa upande wake Mtawala shule za Trust St.Patrick Schools, Bernadinnah Patrick amewataka wazazi kuwa wawazi kuzungumza na watoto wao kuhusu kuwaambia hali halisi ya maisha ilivyo hivi sasa na kamwe wasione aibu kukemea matukio.mbalimbali kwa watoto hao .
“Hapa shuleni kweli tumekuwa tukitengeneza watoto kuweza kujiajiri wakiwa tangu darasa la nne kwa kuwafundisha bunifu mbalimbali ikiwemo upishi,kilimo, kutengeneza sabuni,keki,na mikate na hata biashara zingine ambapo kupitia programu hiyo tayari wanafunzi 40 walienda nchini China kwa ajili ya kujifunza zaidi kwa vitendo kwa wenzetu.”amesema.
Naye Mmoja wa Wakurugenzi shule za Trust .St.Patrick Schools,Mike Patrick Khanya amesema kuwa,tangu kuanzishwa kwa shule hiyo ina miaka 27 sasa na imekuwa ikifanya vizuri kwa wanafunzi katika masomo yote ikiwemo kuinua vipaji vya watoto hao kwa kuwapeleka nje ya nchi kujifunza zaidi kwa vitendo.
Amesema kuwa,shule hiyo ina kituo cha michezo ambapo wamekuwa wakiwasaidia wanafunzi kuweza kufanya vizuri kwenye michezo yao na kuweza kukuza vipaji kwani michezo ni ajira.
Mike amesema kuwa,wamekuwa wakikaa mara kwa mara na watoto wao na kuweza kuwafundisha kuhusu swala zima la mporomoko wa maadili na kuweza kuwafundisha umuhimu wa kujiheshimu na kuzingatia nidhamu .