Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameungana na waumini wengine katika kushiriki Ibada ya Kawaida ya Asubuhi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki Tabora. Makamu wa Rais ameshiriki Ibada hiyo kabla ya kuanza siku ya pili ya ziara ya kikazi mkoani Tabora leo tarehe 09 Oktoba 2024.