Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kushiriki Maonesho ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika viwanja vya Chamanangwe Kisiwani Pemba ikiwa na Teknolojia za Kilimo zinazolenga kumuongezea Mkulima tija.
Waziri Shamata ametoa pongezi hizo leo Oktoba 09, 2024 alipotembelea banda la TARI lenye Teknolojia bora za Kilimo katika mnyororo mzima wa thamani.
Maonesho ya siku ya chakula Duniani mwaka huu yanafanyika yakiwa na kaulimbiu “Haki ya Chakula kwa Wote kwa Maisha bora ya Sasa na yajayo”.
Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Oktoba 10, 2024 Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla.