Na Prisca Libaga Arusha
MLAKA ya Mapato Nchini,TRA,Mkoa wa Arusha ,imevuka malengo kwa kukusanya asilimia 34.05% katikati kipindi cha robo ya kwanza ya ulipaji Kodi kwa hiari katika kipindi cha miezi mitatu ,Julai hadi Septemba mwaka huu.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato,TRA ameyasema hayo jana kwenye Ukumbi wa Mamlaka hiyo kwenye wiki ya mlipa Kodi kuwa mafanikio hayo yanatokana na mchango mkubwa wawalipa kodi na kupongeza ushirikiano huo.
Amesema mafanikio hayo yanatokana na mchango mkubwa wa walipa Kodi mwaka 2023/2024 ambao wamekuwa na mwitikio mkubwa wa ulipaji Kodi kwa hiari bila shuruti
Amesema kuwa ukusanyaji huo wa mapato unachangiwa kwa asilimia 70% ya maboresho ya mfumo ambao unatumika kupokea return ,mfumo ambao unaendelea kuboreshwa na changamoto zilizopo zinaendelea kufanyiwa kazina kupata ufumbuzi.
Amesema TRA,inaendelea kuwashukuru na kuwapongeza walipa Kodi kwa mchango wao wa kulipia Kodi na hii ni wiki ya mlipa kodi hivyo akawaomba walipa Kodi waendelee kutii Sheria bila shuruti katika kulipia Kodi zao .
Kuhusu matumizi matumizi ya mashine za EFD,Dimasi,amesema zinarahisisha ulipaji Kodi na wenye changamoto TRA inawakaribisha milango ya ipo wazi wakati wowote jambo la Kodi ni jambo letu was,pote.
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Fakhruddin Zavery ,ambae ni mshauri wa Kodi Kutoka kampuni ya Hasanali Ruta amesema amekuwa mlipa kodi tangia mwaka 1945 anashukuru kwa heshima hiyo ya kuwa mgeni rasmi kwenye siku ya mlipa kodi anawaomba walipa Kodi wote wenye changamoto washirikiane pamoja ili kutatatua changamoto zinazojitokeza .
Naibu Katibu mkuu taifa wa Chama cha wataalamu na ushauri wa Kodi taifa,Melikizedeki Temba ambae amemwakilishi Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Arusha Nicholaus Duhia,amese walipa Kodi ,amewambia wafanyabiashara kuwa taasisi hiyo inafanya kazi kwa karibu na TRA,ombi ushirikiano uendelee sanjari na maboresho yaendelee kufanyika .