Idara ya afya ya mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini imesema, wanafunzi 74 wa eneo la Rand Magharibi mkoani humo wanapatiwa matibabu kufuatia kuhisiwa kula chakula chenye sumu Alhamisi.
Idara hiyo imesema wanafunzi wa kike takriban 74 kutoka Shule za Sekondari za Fochville, Badirile na ya Ufundi Stadi ya Wedela waliumwa na tumbo na kuharisha waliposhiriki kwenye kambi ya mafunzo.
Taarifa iliyotolewa na idara hiyo imesema wanafunzi wote wanaoumwa wamepelekwa hospitali kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi, na wengi wao wako sasa wana hali nzuri.
Katika siku za karibuni Afrika Kusini imeshuhudia matukio mengi ya sumu kwenye chakula miongoni mwa watoto. Wikiendi iliyopita, watoto watano walikufa kwa kuhisiwa kula chakula chenye sumu huko Naledi, Johannesburg. Siku ya Jumatano, wanafunzi 35 kutoka Malamulele, Mkoa wa Limpopo, walipelekwa hospitalini kufuatia kuhisiwa kula chakula chenye sumu.
The post Wanafunzi 74 walazwa hospitali kutokana na kuhisi kula chakula chenye sumu Afrika Kusini first appeared on Millard Ayo.