Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoani Mara limewasha umeme na kugawa mitungi ya gesi kwa akina mama wajasilia Mali na wauzaji wa maziwa katika Kijiji cha Nnyanungu Wilayani Serengeti Mkoani mara ikiwa nikampeni maalum ya kupinga matumizi ya nishati kuni
Akizungumza Meneja wa Tanesco Mkoani wa Mara Nickson Babu alisema kwa Muda mrefu Kijiji hicho kimekuwa na changamoto ya Umeme ambapo wakazi pamoja na akina mama wanaojihusisha na uuzaji wa maziwa wamekuwa wakilazimika kutumia kuni za kuchemshia maziwa Jambo ambalo limekuwa likihatarisha Afya zao.
“Tumewasha umeme nakuleta mitungi ya gesi kwa akina mama katika Kijiji hiki hususan katika kikundi cha uuzaji wa maziwa hii itasaidia kulinda Afya za Wanawake hawa ambao walikuwa wakitumia nishati ya kuni ambayo nihatari kwa Afya zao”Nickson Babu Meneja wa Tanesco Mara.
Babu amesema ukataji Miti kwa ajili ya shughuli za nyumbani umekuwa changamoto kubwa katika maeneo yao kutokana na kuwa kando na hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo kwa Muda mrefu imekuwa ikihatarisha Usalama wawananchi kuingia hifadhini nakutokana na uwepo wa wanyama wakali.
Nao baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nnyanungu wameishukuru Shirika la Umeme Tanzania Tanesco kwa kuwakukbuka na kuwaondolea adha ya ukosefu wa nishati hiyo iliyodumu kwa Muda mrefu ambapo uwepo wa Gesi na umeme utasaidia kufanya shughuli zao kwa urahisi tofauti na kipindi cha nyuma ilivyokuwa.