Mkurugenzi wa Bodi ya Amana DIB Bw. Isack Kihwili, (katikati) akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda hilo Leo ili kupata elimu juu ya shughuli za bodi katika maonesho ya teknolojia ya madini yaliyofungwa Leo ma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita ambapo katika kipindi cha siku kumi za maonesho hayo zaidi ya watu 400 walihudumiwa na kupata elimu, (kushoto) ni Mhasibu Mwandamizi wa taasisi hiyo Bi. Kulwa James Kasuka na kulia ni Caren Max Afisa wa Bodi ya Bima ya Amana.
Wananchi waliofika katika banda hilo Leo ili kupata elimu juu ya kazi zinazozifanywa na Bodi hiyo katika maonesho ya teknolojia ya madini yaliyofungwa Leo kwenye viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita (kushoto), ni Mhasibu Mwandamizi wa DIB .
Caren Max Afisa wa Bodi ya Bima ya Amana akitoa maelezo kwa wananchi waliofurika bandani hapo kupata elimu ya Mambo mbalimbali yanyofanywa na Bodi hiyo.
Baadhi ya wanafunzi mbalimbali waliofika bandani hapo wakipiga picha ya pamoja Mara baada ya kuelimishwa kuhusu kazi za DIB.
Caren Max Afisa wa Bodi ya Bima ya Amana akitoa zawadi kwa wananchi waliofurika bandani hapo kupata elimu ya mambo mbalimbali yanyofanywa na Bodi hiyo.