-NIC yaweka mikakati ya kutoa elimu ya Bima nchini
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.
NIC Insurance imeshinda Tuzo ya kibabe katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii na Bima katika Maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini yaliyokuwa yakifanyika mkoani Geita.
Akizungumza wakati wa Kukabidhi Tuzo ya Ushindi huo Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa ushindi wa NIC unatokana huduma bora ya bimacl katika kuhudumia sekta ya madini.
Mavunde amesema kuwa katika maonesho hayo NIC imekuwa mdau muhimu kwa kuunganika na wengine katika kuonesha na kutoa huduma.
Amesema kuwa wafanyabuashara wa madini wameweza kupata elimu ya bima na watakuwa wadau wa NIC kwa kukata Bima kwa ajili ya kinga katika majangai
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo ya Ushindi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Mkurugenzi Masoko na Uhusiano wa NIC Insurance Karim Meshack amesema kuwa ushindi huo unafanya kuendelea kujiimarisha zaidi katika kutoa huduma za bima nchini.
Amesema kuwa wafanyabiashara ya Madini na Wachimbaji wa Madini kutumia Bima za NIC katika kulinda mitaji katika majanga mbalimbali.
Sekta ya madini ina uwekezaji mkubwa hivyo kukata Bima ya NIC Insurance kuna kufamya kuwa huru kuwa pindi ya majanga yakifika NIC inafuta machozi kwa Tishu kwa uwezo wake wa kulipa mafao na kuendelea na shughuli za madini.
Amesema NIC katika maonesho hayo wametoa elimu ya bima pamoja na faida za bima kutokana tafiti walizo nazo ili kila mdau wa madini awe na uelewa wa bima.
Meshack amesema NIC inataka wadau wa madini kukata bima ya NIC katika kufanya biashara hiyo kwa uhakika.
Amesema Watanzania wamewapa dhamana NIC katika kuwalinda katika majanga yanayowakuta kutatuliwa na bima.
Meshack amesema mfanyabiashara wa madini kawekeza bilioni 1 linatokea janga katika mgodi anapoteza fahamu wakati NIC ipo kwa ajili ya kulinda bilioni moja iliyowekezwa.
Amesema katika bidhaa za bima watanzania wanaweza kukata bima ya maisha ambapo ikitokea baba au mama ambao wako katika biashara ya madini walikata bima ya NIC itatoa bima kwa familia iliyobaki katika kuendesha maisha na kufanya waliofiwa kulia kwa kuondokewa na mtu lakini maisha yao yataendelea kama kawaida.
Aidha amesema bidhaa nyingine ya Bima ni Beam Life na uwekezaji ambapo aliyekata atafapata faida ya asilimia Saba kwa mwaka.
Meshack amesema aliyekata Bima ya Beam Life akifariki NIC itatoa mkono wa pole asilimia 5 ambayo haitoki kwenye fedha aliyoweka.
Hata hivyo amesema kuwa wamekwenda mbali kwa kugusa sekta ya madini kwa kuwa na bima ya madini ambayo inamlinda mfanyabiashara katika kumuondolea hofu ya gharama za zake uwekezaji likitokea janga NIC kufanya fidia ya kuendelea na biashara ya madini.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akikabidhi tuzo ya Ushindi kwa NIC
Insurance katika maonesho ya Teknolojia ya Sekta ya Madini mkoani
Geita.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo kwa NIC Insurance.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Karim Meshack ‘ Black T-Shirt’ akiwa katika picha ya pamoja timu ya NIC katika maonesho ya saba ya Teknolojia mkoani Geita.
Wafanyakazi wa NIC Insurance wakiwa katika nyuso za furaha wakiwa na cheti na tuzo mara baada ya kuibuka washindi katika maonesho ya saba ya Teknolojia ya sekta ya Madini mkoani Geita.