Diwani wa Kata ya Mikocheni Eng. Nzenzely Hussein Ajiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura, Atoa Wito kwa Wananchi Kujitokeza kwa Wingi
Dar es Salaam, Oktoba 14, 2024 – Diwani wa Kata ya Mikocheni, Eng. Nzenzely Hussein, amejitokeza rasmi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wa Serikali za Mitaa, huku akiwahimiza wananchi wa Mikocheni na Tanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo muhimu.
Akizungumza mara baada ya kujiandikisha, Eng. Nzenzely Hussein aliweka msisitizo juu ya umuhimu wa kila mwananchi kutumia haki yake ya kidemokrasia kwa kuhakikisha anajiandikisha ili kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ujao. Alibainisha kuwa ushiriki wa wananchi katika uchaguzi ni hatua muhimu ya kuhakikisha wanapata viongozi wanaowajibika na wenye kujali maslahi ya jamii.
The post Kauli ya Diwani wa Mikocheni Eng.Nzenzely baada ya kujiandikisha daftari la wapiga kura “Ni haki yako” first appeared on Millard Ayo.