Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024,Godfrey Mzava amesema leo, baada ya kuweka jiwe la msingi katika wodi ya Mm na Mtoto katika Zahanti ya Nyakato, wilyani Ilemela.
Amesema katika miradi yote Mwenge ulikopita kuweka mawe ya msingi,kukagua na kufungua baadhi,umeridhika kwa namna ilivyotekelezwa kwa ubora na kwa usimamizi mzuri, hivyo wameitendea haki fedha ya serikali,michango ya wananchi na wadau wa maendeleo.
“Kote tulikopita kwenye miaradi,tumekuta wananchi wamejitokeza kwa wingi kuja kuulaki Mwenge wa Uhuru lakini pia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Nakupongeza wewe kiongozi wetu wa shughuli za serikali wilayani kwetu kwa namna ulivyoyaunganisha makundi ya kijamii na kisiasa, ndio maana miradi ya maendeleo imefanikiwa,”amesema Mzava.
Amesema mafanikio ya utekelezaji wa miradi hiyo unadhirisha Ilemela anapewa ushirikiano wa kutosha na viongozi wengine wilayani huko, watumishi na wananchi.
“Tumeona utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ni dhahiri tusingeweza kupita katika miradi yote kazi inayofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025,ni imani yetu kuwa miradi yote imetekelezwa kwa viwango na ubora ule ule,”amesema Mzava.
Mwenge huo wa Uhuru uliweka jiwe la msingi katika jengo la wodi ya Mama na Mtoto la Zahati ya Nyakato lililogharimu sh. milioni zaidi ya 227.9 za serikali kuu, mapato ya ndani na wananchi,pia umefungua bweni la watoto wenye mahataji maalum katika shule ya Msingi Buswelu,lililogharimu sh. milioni 172 zikiwemo za mapato ya ndani na serikali.
Aidha umezindua mradi wa maji katika shule ya sekondari Bwiru wavulana, uliojengwa kwa gharama ya sh. milioni 31.548 kwa ushirikiano kati ya The Desk & Chair Foundation (sh.milioni 19.75 na halmashauri ya Ilemela sh. milioni 11.798 za mapato ya ndani),
Mwenge wa Uhuru pia umezindua shule ya sekondari Kisenga iliyogharimu milioni 584.28 na mradi wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule hiyo wenye thamani ya sh. milioni 380,kituo cha mafuta cha GBP kilichogharimu sh.milioni milioni 520 na barabara ya Kiyungi sh.milioni 499.655.