Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati akiwasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (km 3) na barabara unganishi (km 1.66) kwa kiwango cha lami Mkoani Mwanza leo tarehe 13 Oktoba, 2024. Ujenzi wa Daraja hilo umefikia asilimia 93.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (km 3) na barabara unganishi (km 1.66) ambao umefikia asilimia 93 Mkoani Mwanza leo tarehe 13 Oktoba, 2024.
Mwonekano wa ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) Kilometa 3 linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara – Sengerema – Geita kupita Ziwa Victoria na ujenzi wa barabara unganishi zenye urefu wa Kilometa 1.66 ambapo utekelezaji wake unaendelea na umefikia asilimia 93 Mkoani Mwanza, leo tarehe 13 Oktoba 2024. (PICHA NA WU)