Maonesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) mwaka 2024 yamehitimishwa rasmi jijini Dar es Salaam, yakiteka hisia za wengi kwa mafanikio makubwa ya kuingiza takribani wanunuzi 120 wa kimataifa wa bidhaa za utalii.
Katika hafla ya kufunga maonesho hayo kwenye ukumbi wa Mlimani City, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana, alieleza kuwa mwitikio wa washiriki umeongezeka, akitaja filamu maarufu ya “The Royal Tour” aliyotengeneza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama kichocheo muhimu.
“Utalii unachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa, kuanzia pale mtalii anaposhuka uwanja wa ndege, hadi anapohudumiwa na hoteli na kufanya shughuli mbalimbali,” alisema Dkt. Chana.
Pia katika maonesho hayo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) iliweza kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali pamoja na kupoke mapendekezo au changamoto wanazozipitia wakati wa kutumia miundombinu ya Mamlaka hiyo.
Afisa Masoko kutoka TAA Shaaban Towo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Kitengo cha Undeshaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal 3 Keneth Lwejuna aliyetembelea Banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwenye maonesho ya Nane ya Swahili International Tourism Expo (S!TE 2024) katika Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka TAA Mariam Lussewa akitoa maelezo kuhusu Mamlaka hiyo pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali kwa mwananchi aliyetembelea banda la Mamlaka hiyo kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya Nane ya Swahili International Tourism Expo (S!TE 2024) katika Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mary Mushi akitoa maelezo kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyojikita katika kusimalia Viwanja vya ndege pamoja na fursambalimbali ziliopo katika Usafiri wa Anga wakati wa maonesho ya Nane ya Swahili International Tourism Expo (S!TE 2024) katika Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
Afisa Masoko kutoka TAA Shaaban Towo (wa pili kulia) akitoa maelezo kuhusu namna fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya Usafiri wa Anga kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwenye maonesho ya Nane ya Swahili International Tourism Expo (S!TE 2024) katika Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
Afisa masoko kutoka TAA Abrahaman Dilunga akitoa maelezo kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakati wa maonesho ya Nane ya Swahili International Tourism Expo (S!TE 2024) katika Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
Afisa Masoko TAA Kasanga Festo pamoja na Afisa Masoko kutoka TAA Shaaban Towo wakimsikiliza mmoja wa wananchi waliofika kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya Nane ya Swahili International Tourism Expo (S!TE 2024) katika Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
Maonesho yakiendelea
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAkA) wakiwa kwenye banda la Mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya Nane ya Swahili International Tourism Expo (S!TE 2024) katika Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.