SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma,inatarajia kumfikisha mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA),Prof.Eliamini Sedoyeka kwa tuhuma za ukiukwaji wa Sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Maadili,Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi,imesema baraza hilo linatarajiwa kufanya kikao cha uchunguzi wa kina wa malalamiko hayo kwa mujibu wa kanuni ya 11 ya kanuni za maadili ya viongozi wa umma,mwaka 20217.
Kikao hicho kitafanyika saa tatu asubuhi kuanzia Oktoba 16 hadi 17,2024 Jijini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mtaa wa TAMBUKARELI Makao Makuu DODOMA.
Taarifa hiyo imesema uchunguzi huu wa wazi unafanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (5) na 29 (6) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Aidha, wananchi wote mnaalikwa kuhudhuria katika kikao hicho muhimu.