Meneja Mkuu wa kampuni ya utalii ya Classic Tours & Safaris , Beatrice Dimitris Dallaris akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo
……………
Happy Lazaro, Arusha .
Wadau mbalimbali wa utalii mkoani Arusha wamepongeza uwepo wa tamasha la Landrover Festival kwa mkoa wa Arusha kwani umeleta fursa nyingi kwa wadau ikiwemo kutangaza magari yao kwa wadau wa ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa kampuni ya utalii ya Classic Tours & Safaris , Beatrice Dimitris Dallaris wakati akizungumza na waandishi habari kwenye tamasha hilo katika viwanja vya magereza mkoani Arusha.
“Uwepo wa tamasha hilo umeleta fursa nyingi za kuweza kukutana na kufahamiana na watu mbalimbali waliotoka Mikoa mbalimbali na pia Nchi za jirani kikubwa zaidi ni kwa Mkurugenzi Mkuu wa sasa wa kampuni ya Classic Tours & Safaris , Joan Auye Melleo Mrema ambae ametumia nafasi hii kumuenzi na kumkumbuka Marehemu Baba yake Mpendwa Melleo Auye Mrema aliefariki mwezi July 2017 ambae ndie Mwanzilishi wa kampuni hiyo ya utalii aliyoianzisha mnamo mwaka 2004. “amesema.
Beatrice amefafanua kuwa, kupitia tamasha hilo la Land Rover Festival tumepata fursa ya kuweza kuonyesha moja ya gari la kampuni yetu la aina ya Landrover 110 “EXTENDED” yenye usajili wa number T207ABD sambamba na kuendelea kuitangaza kampuni yetu kwa wadau mbalimbali kutoka la ndani na nje ya nchi.
“Kipekee nampongeza sana Rais wetu Daktari Samia Suluhu Hassan kupitia Mkuu wa Mkoa wetu wa Arusha Paul Makonda ambaye aliweka baraka zake za kipekee kwa kuruhusu hili jambo kuweza kufanyika katika mkoa wetu wa kitalii wa Arusha na kuweza kuvunja rekodi ya dunia” sio hivyo tu kwa kutuonyesha kwa vitendo upendo wake katika sekta ya UTALII kupitia filamu yake ya ROYAL TOUR na Sisi tumeneemeka kwani mbali na kuwa na kampuni ya kuendesha watalii pia tunamiliki hotel ya kimataifa ya Ngurdoto Mountain Lodge ambayo ipo ndani ya Mkoa wetu wa Arusha amesema Beatrice
Ameongeza kuwa, tamasha hilo limeweza kuinua kiwango kikubwa cha kipato kwa wawekezaji wa aina zoote na kwa maeneo mbalimbali kwa wakati mmoja kwani idadi kubwa ya watanzania kutoka mikoa mbalimbali na wageni kutoka nje ya nchi waliweza kufika na kutembelea kwenye mbuga yetu ya Arusha National Park na maeneo mbalimbali ya Mkoa wetu wa Arusha na kujionea mambo mengi na ya mbalimbali yaliokuwepo.
Amefafanua zaidi kuwa, ni vizuri matamasha kama hayo na ya aina nyingine yakawepo mara kwa mara ili kuchangamsha Mkoa wetu na pia kutoa fursa kwa wadau mbalimbali kuweza kujitokeza na kuonyesha ubunifu wao na bidhaa zao ili kuendelea kufahamika zaidi ndani na nje ya Nchi yetu.
Aidha amesema kuwa ,Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa Mikoa ya Tanzania iliyobarikiwa kwa ASALI NA MAZIWA.