Shirika la Afya Ulimwenguni –WHO lilisema Jumatatu kuwa limeidhinisha chanjo mpya ya mpox BAVA.CO kwa vijana wenye umri wa miaka 12 hadi 17, kundi linalotajwa kuwa katika hatari kubwa ya milipuko ya ugonjwa huo ambao umezua wasiwasi ulimwenguni.
WHO ilisema katika taarifa yake kwamba ilitoa kibali cha awali cha chanjo hiyo ya Jynneos kwa vijana Oktoba 8.
WHO ilitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya umma duniani kwa mara ya pili ndani ya miaka miwili mwezi Agosti baada ya aina mpya ya virusi kuenea kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hadi kwa majirani zake.
The post WHO yaishinisha chanjo mpya ya Mpox first appeared on Millard Ayo.