Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)imeshiriki Kongamano la pili la Kimataifa katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji Oktoba 17, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo ambalo litajadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuiinua sekta nzima ya uchukuzi na usafirishaji limefunguliwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Profesa Mbarawa ameelekeza menejimenti ya Chuo cha Usafirishaji (NIT) kuanza kutumia ndege mbili zilizonunuliwa na serikali kwaajili ya kufundishia marubani ili taifa liweze kutumia rasilimali hiyo ambayo ina uhaba mkubwa nchini.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi amesema Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kipo katika hatua za mwisho za ukaguzi ili kipatiwe cheti kitakacho wawezesha kutoa mafunzo ya Urubani yenye vigezo vya Kimataifa, hivyo chuo kitimize mahitaji yote stahiki ili waweze kupatiwa ithibati ya kutoa mafunzo hayo.
Aidha, Mkuerugenzi Mkuu Msangi amesema chuo cha NIT kimejikita zaidi katika kutoa kozi za muda mrefu, wakati TCAA nayo ina chuo chake cha Usafiri wa Anga (CATC) kinatoa kozi za muda mfupi, vyuo vyote vikiwa na lengo la kukabiliana na changamoto ya upungufu wa wataalam wa sekta ya usafiri wa anga nchini.
Kongamano hilo lililoandaliwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji linafanyija kwa siku tatu likiunganisha wadau mbalimbali wa toka ya Uchukuzi na Usafirishaji nchini.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi alipokuwa akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) wakati wa Kongamano la pili la kimataifa katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji, lilofanyika Oktoba 17, 2024, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa kufungua kongamano la pili la kimataifa katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji lililofanyika leo Oktoba 17, 2024, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau kutoka sekta ya uchukuzi na usafirishaji wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa kongamano la pili la kimataifa katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji lililofanyika Oktoba 17, 2024, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akisaini kitabu katika banda la Mamlaka hiyo wakati wa kongamano la pili la kimataifa katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji lililofanyika Oktoba 17, 2024, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara ya Uchukuzi wakati wa kufungua kongamano la pili la kimataifa katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji lililofanyika Oktoba 17, 2024, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo katika kongamano la pili la kimataifa katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji lililofanyika Oktoba 17, 2024, jijini Dar es Salaam.