Rais William Ruto amemteua Naibu Rais mpya baada ya Rigathi Gachagua kuondolewa na Bunge la Seneti.
“Rais William Ruto amependekeza na kulipeleka bungeni jina la Profesa Kithure Kindiki kama Naibu Rais,” taarifa ya Ikulu ya Kenya imesema.
“Iwapo itaidhinishwa, Waziri wa Mambo ya Ndani atamrithi Rigathi Gachagua ambaye alitimuliwa na Seneti siku ya Alhamisi,” imeongeza kusema taarifa hiyo
Kindiki ni mwanasiasa wa Kenya na wakili maarufu ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa.
Alizaliwa Julai 16, 1972 huko Tharaka, kaunti ya Tharaka Nithi.
“Spika, umewasilisha ujumbe kutoka kwa Rais Ruto kuhusu uteuzi wa Kithure Kindilki kujaza nafasi ya ofisi ya Naibu Rais.
.
The post Kithure Kindiki, ateuliwa kuwa Naibu Rais Kenya first appeared on Millard Ayo.