Mlinda mlango wa Manchester City Éderson amesema anafikiri klabu yake tayari imepanga mrithi iwapo Pep Guardiola ataamua kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Guardiola, mwenye umri wa miaka 53, hivi majuzi alikiri kuwa hajafanya uamuzi iwapo ataendelea kuinoa City zaidi ya Juni 2025, mkataba wake utakapokamilika.
“City ni klabu yenye muundo mzuri, inasimamiwa vyema, ina wakurugenzi wazuri, Mkurugenzi Mtendaji mkuu, kocha mzuri,” Éderson aliambia TNT Sports Brazil.
“Naamini klabu tayari ina meneja ajaye akilini mwake… siku Pep akiamua kuondoka watajaribu kufuata mkondo huo huo, bila shaka itakuwa hasara kubwa, sina shaka na hilo kwa sababu upo. nikizungumza kuhusu kocha bora zaidi duniani naona klabu iliyoandaliwa vyema kwa ajili ya [zama] za baada ya Guardiola.”
The post Man City wametayarisha mbadala wangu – Éderson first appeared on Millard Ayo.