Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akizungumza wakati wa Mahafali ya 13 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Jacob Kibona akizungumza katika Mahafali ya 13 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB kuanzishwa kwa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi 2007 nak usema kuwa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha bodi matokeo yote ya mitihani ya bodi ni lazima yapitiwe na kuidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi.
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa Mahafali ya 13 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB ambapo amewaasa wahitimu kufanya kazi kwa kufata maadili ya kitaaluma ili kulinda heshima ya fani yao na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasirimali za umma kwa manufaa ya Taifa wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Mshehereshaji ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akizungumza jambo wakati wa Mahafali ya 13 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB.
Baadhi ya Wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa PSPTB wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) wakati wa Mahafali ya 13 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya Bodi wakati wa mahafali ya 13 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akiwatunuku wahitimu wa walioudhuria Mahafali ya 13 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Sheria PSPTB Piencia Kiure akiwaapisha Wahitimu wa mahafali ya 13 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kiapo cha kiapo cha utii, uadilifu na uaminifu
Wahitimu wa mahafali ya 13 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakila kiapo cha utii na uaminifu
Picha mbalimbali za pamoja katika mahafali ya 13 ya wahitimu wa mitihani ya kitaaluma ya PSPTB