Wanafunzi wa shule ya sekondari Mwambola,Dadas Rise wakiwa wameshika taulo za kike
Na Hellen Mtereko,
Mwanza
Zaidi ya wanafunzi 80 wa kike katika shule ya sekondari Mwambola Wilayani Misungwi,Mkoani Mwanza wamepewa msaada wa taulo za kike ili kuwanusuru na changamoto ya kushindwa kuhudhuria masomo.
Akizungumza leo Octoba 18, 2024 mara baada ya kupokea msaada huo uliotolewa na Mashirika yanayoongozwa na wanawake vijana (Dadas Rise) Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mtoto wa kike, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Joseph Bujiku alieleza kuwa ukosefu wa taulo za kike unachangia kwa kiasi kikubwa watoto kuwa watoro.
“Mtoto anapopata hedhi akiwa shuleni anashindwa kujistiri hivyo analazimika kurudi nyumbani na wengine wanaamua kukaa kabisa hadi hedhi iishe ndio aanze kuja shule kwahiyo ukosefu wa taulo unachochea utoro na unawafanya watoto washinde kujiamini”, alisema
Kwaupande wake Afisa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Dayana Kuboja alisema baadhi ya familia hazina uwezo wa kuwanunulia watoto wao taulo hizo hivyo amewaomba wadau wengine na mashirika kujitokeza kusaidia wasichana waweze kujistri.
Mariam Samweli ni mmoja wa wanafunzi walionufaika na msaada huo alisema utawasaidia kujistri vizuri na kuachana na nyenzo nyingine kama vitambaa.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Teens Corridor, Sophia Nshushi alisema wametoa msaada huo ili kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma katika mazingira salama hususani wanapokuwa kwenye kipindi cha hedhi.
“Pamoja na msaada huo tulioutoa pia tumeweza kuwapa elimu ya uongozi kuanzia ngazi ya shule na baadae katika ngazi ya serikali za mitaa,
Nshushi alitumia fursa hiyo kuishukuru taasisi ya The Desk and Chair kwa kuwawezesha badhi ya taulo za kike ambazo wamezitoa kwa wanafunzi hao.
Anitha samsoni kutoka Shirika la Hope for Youth Development, alisema wataendelea kutoa elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi ili waweze kuwa na uelewa wa suala hilo.
Esther Moris kutoka shirika la naweza tena alieleza kuwa taulo za kike zinawasaidia wasichana kuwa na utulivu pindi wanapokuwa kwenye hedhi.
Mashirika yanayoongozwa na WA awake vijana (Dadas Rise) Mkoa wa Mwanza wakiwa katika shule ya sekondari Mwambola kwaajili ya kutoa taulo za kike
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mwambola,Dadas Rise wakiwa wameshika taulo za kike.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mwambola Joseph Bujiku akigawa taulo za kike kwa wanafunzi