Kikao hicho kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 20 Oktoba 2024 na kilihudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania ambayo ni Mwenyekiti wa Organ; Malawi Mwenyekiti ajaye na Zambia ambayo ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake na Sekretarieti ya SADC.
Kikao kimepokea na kujadili taarifa iliyowasilishwa na Sekretarieti ya SADC kuhusu maandalizi ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Botswana utakaofanyika tarehe 30 Oktoba,2024.
Sekretarieti pia iliwasilisha mgawanyo wa majukumu kwa timu mbalimbali za misheni hiyo katika uchaguzi huo.
Katika kikao hicho Mhe. Pinda amesema ni matumaini yake kuwa maandalizi na Mipango ya Uangalizi itaenda sawa na hivyo kuifanya SEOM kutekeleza jukumu lake kwa tija na ufanisi.
Amesema pia SEOM ıkifanya kazi yake ya uangalizi na kuandaa taarifa za Uangalizi wa uchaguzi huo itasaidia nchi husika kufanya maboresho katika mifumo yake ya demokrasia na hivyo kuwa sehemu ya kukuza demokrasia katika nchi wanachama.
Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Botswana (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda
akipokea taarifa ya mandalizi ya uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Botswana
kutoka kwa Sekretarieti ya SADC jijini Gaborone Botswana tarehe 20
Oktoba, 2024
Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini Botswana (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda
akiwa na wajumbe wa timu ya uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Botswana
wakipokea taarifa ya maadalizi ya uangalizi wa uchaguzi kutoka kwa Sekretarieti ya SADC jijini Gaborone Botswana tarehe 20
Oktoba, 2024
taarifa ya maandalizi ya uangalizi ya uchaguzi mkuu wa Botswana kwa Mkuu
wa Misheni ya SADC ya kuangalia uchaguzi mkuu wa Botswana Mhe. Mizengo
Pinda hayupo pichani