Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi za Kiraia (FCS) Bw. Justice Rutenge (kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) Bw. Daud Daudi katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano ya miaka mitatu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa walaji na haki katika sekta ya usafiri ardhini iliyofanyika leo Oktoba 22, 2024 Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw. Justice Rutenge akizungumza jambo katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano ya miaka mitatu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa walaji na haki katika sekta ya usafiri ardhini iliyofanyika leo Oktoba 22, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Bw. Daud Daudi akizungumza jambo katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano ya miaka mitatu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa walaji na haki katika sekta ya usafiri ardhini iliyofanyika leo Oktoba 22, 2024 Jijini Dar es Salaam.
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Asasi za Kiraia (FCS) imesaini mkataba wa makubaliano wa miaka mitatu na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa walaji na haki katika sekta ya usafiri ardhini kwa kuwajenga uwezo katika kutafuta rasilimali za kutekeleza mipango.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano kati ya FCS na LATRA CCC iliyofanyika leo Oktoba 22, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw. Justice Rutenge amesema kuwa lengo la mkataba huo kuinua sauti za walaji kwa kuwezesha mabaraza kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao.
“FCS na LATRA CCC tumekusudia kuunda mazingira bora ya walaji katika sekta ya usafiri wa ardhi, kukuza utaratibu bora za kibiashara pamoja na kuhamasisha ukuaji wa biashara” amesema Bw. Rutenge.
Amesema kuwa ushirikiano huo utakwenda kubuni na kutekeleza mipango inayokuza haki za walaji na kulinda bidhaa na huduma za usafiri wa ardhi zinazodhibitiwa ikiwemo barabara, reli na majini.
Ameeleza kuwa LATRA CCC ni wadau muhimu katika kukuza ulinzi wa walaji katika sekta ya usafiri wa ardhi, huku akieleza kuwa FCS itatumia utaalamu wake katika kujenga uwezo kusaidia LATRA CCC katika kutafuta rasilimali za kutekeleza mipango inayolenga kulinda haki za walaji nchini.
“Haki muhimu za walaji ni haki ya kupata malipo ya haki kwa madai, elimu kuhusu usafiri wa ardhini, bidhaa na huduma pamoja na uhakikisho wa ubora” amesema Bw. Rutenge.
Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Bw. Daud Daudi amesema kuwa ulinzi wa walaji katika sekta ya usafiri ni muhimu, huku akisisitiza ushirikiano kati ya wadau wa maendeleo ili kuimarisha mifumo ya ulinzi kwa walaji pamoja na kuhakikisha kunakuwa na hatua madhubuti.
Amesema kuwa FCS na LATRA CCC wanatarajia kutekeleza mpango wa ulinzi na haki za walaji katika sekta ya usafiri nchini Tanzania kwa kukuza uwezo wa walaji, kutetea haki zao na kuimarisha ushirikiano na wadau muhimu.
“Ushirikiano wa FCS na LATRA CCC unalenga kufikia malengo kwa kuhusisha jamii na baraza la udhibiti kupitia ushirikiano na wadau muhimu kwa kuanzisha kamati za walaji maalum kwa ajili ya maeneo ya Kisekta.