Mkaguzi Kata ya Kisangura Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Genuine Kimario amewaomba wanafunzi waliohitimu elimu ya kidato cha nne kuendelea kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili.
Mkaguzi huyo ameto rahi hiyo wakati alipokaribishwa kitoa neno kwa wahitimu hao ambao wapo katika Kata ambayo ana hihudumu ambapo amewataka wanafunzi Kuendelea kuwa mabalozi wa kupaza sauti ya vitendo viofu katika Jamii.
Aidha Kimario amewasihi wanafunzi hao na kuwataka kutambua kuwa safari yao bado ni ndefu akiwataka kutambua bado safari yao kimasomo ni ndefu huku akiwataka kutokubali kurubuniwa na watu wenye nia ovu.
Vile amewaomba kipindi chote ambacho watakuwa wanasubili matoke wawe mabalozi wazuri katika masuala ya ulinzi huku akiwataka kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi.