Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulia Mafuta na Gesi Dkt James Mataragio akizungumza wakati alipofungua Kikao cha Pili cha Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi PURA.
Mkurugenzi wa PURA Mhandisi Charles Jimmy na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la PURA akizungumza wakati wa kikao hicho
Na Oscar Assenga, TANGA.
WIZARA ya Nishati imesema kwamba wana mpango wa kunadi vitalu vya utafutaji wa Mafuta na Gesi asili nchini pamoja na kuingia makubaliano ya uzalishaji na makampuni ya nje.
Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulia Mafuta na Gesi Dkt James Mataragio Octoba 21 mwaka huu wakati wa Kikao cha Pili cha Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi PURA.
Ambapo alisema hiyo itakuwa ni raundi ya tano na zimeshafanyika raundi nne tokea mwaka 2000 na raundi ya 5 itafanyika mwaka kesho itayokwenda sambamba na mkutano wa Kimataifa wa East African Petroli Conference and Exibition ambao utajumuisha nchi zote za Jumuiya ya Africa Mashariki
Alisema kwamba mkutano huo unatazamiwa kufanyika Machi 5 mwaka Dar es Salaam na wanatarajia mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt Samia Suluhu kwa ajili ya kuzindua vitalu na watavinadi vitalu 24 ambavyo wanapanga kuvinadi huku wakiwakaribisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuangalia vitalu.
Aidha alisema kwamba wameingia mkataba na kampuni ya TGS ambao wameingia mkataba wa kufanya masoko ya vitalu na Serikali imejipanga vizuri na kikubwa kuwa na uwazi na utayari na wizara imejipanga kushirikiana na Pura ambao ndio msimamizi wapo nao pamoja katika zoezi la kunadi vitalu hivyo.
“Tunategemea katika jitihada zinazofanywa sasa tunaanza kuitangaza nchi kwenye sekta ya mafuta na hivi karibu mtaona makapuni mengi yanakuja Tanzania na tuna miradi mikubwa ya kuchakata gesi unaofanyika Lindi ni miradi tunayoitangaza”Alisema
Alisema kwamba hiyo yote inaonyesha mazingira bora yaliyopo nchini ya uwekezaji kwa sababu mwekezaji anaposikia nchi ina mradi wa Dola Bilioni 42 ambao unataka kufanyika Tanzania anakuwa na imani kwamba sheria zetu,vivutio vyetu vya kifedha, taasisi zetu zinauwezo hivyo wawekezaji wakija nchini na kuwekeza uwekezaji wao utakuwa salama.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukinadi vitalu vyetu na kujitahidi kuhakikisha kunadi vitalu pamoja na kuingia makubaliano ya uzalishaji na makampuni ya nje mara ya mwisho tulinadi vitalu 2013 na kukaa muda mrefu bila ya kufanya hivyo kutokana na sababu mbalimbali ikwemo ni takwa ya kisheria”Alisema
Alisema kwa sababu njia ya shearingi ya mwaka 2013 ilikuwa haisomani na sheria ya mafuta ya mwaka 2015 na sasa walichokifanya kama wizara wamebadilisha mkataba wa mauzo wa mfumo wa uzalishaji ambao itasadia kwenda kujadili mikataba mbalimbali ya uwekezaji kwenye upande wa mafuta na itatoa vivutio vyingi itakayowasaidia kampuni za kimataifa za mafuta kuja kuwekeza Tanzania,
Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mkurugenzi wa PURA Mhandisi Charles Jimmy na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la PURA alisema kwamba watanadi vitalu na ambacho kinachofanyika kwa mujibu wa sheria na wao wanasimamia kwa sasa Tanzania ukichukua eneo lake la kilomita za mradi 947,000 kiasi cha eneo la mraba 534,000 zinaonyesha viashiria vya kuwa na mafuta au gesi asilia.
Aidha alisema kati ya hizo ni 534,000 wana 162,000 ambazo tayari zimeshafanyiwa kazi sawa na asilimia 30 na vitalu 21 vitatoka bahari kuu na vitatu vitatu vitatoka upande wa Ziwa Tanganyika na watavitangaza na watu watatoa mapendekezo ya kuvifanyia kazi.
Alisema kwamba watazingitia vigezo vilivyowekwa pamoja na nchi itapata nini kutokana na mapendekezo yao na baadae watachagua aliyebora wampe vitalu kimoja, viwili au vitatu ili aendelee kufanya utafiti na wao watasimamia tafiti hizo.