*Rukwa ,Morogoro vinara katika ulaghai wa simu za mkononi
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imesema idadi ya dakika za huduma ya sauti ndani na nje ya mtandao nchini kwa robo ya mwaka inayoishia Juni 2024 na Septemba 2024 imeonesha zilitumika dakika bilioni 39.6 na kufikia Septemba mwaka huu zilitumika dakika bilioni 41.1.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya robo tatu inayotoa takwimu za mawasiliano za robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024 wa mwenendo wa mawasiliano nchini Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta Mhandisi Felician Mwesigwa amesema kuwa mwenendo huo unatoa fursa ya uwekezaji kutokana mahitaji katika huduma hizo.
Mhandisi Mwesigwa amesema kuwa taarifa za mwenendo huo wanaangalia matika maeneo matatu ambayo ni Simu na Internet ,Utangazaji pamoja na Posta.
Felician alisema Idadi ya dakika za huduma ya sauti ndani ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita imeongezeka kwa wastani wa wastani wa asilimia 9.
Amesema hadi kufikia Septemba 2024 kulikuwa na jumla ya minara 8,583 katika mkoa wa Dar es Salaam, ikifuatiwa na mkoa wa Mwanza yenye minara 423.
Aidha alisema mikoa yenye idadi ndogo zaidi ya minara kwa Tanzania Bara ni Katavi 94 na Songwe 108.
Amesema kwa upande wa Tanzania Visiwani, Mkoa wa Mjini Magharibi una idadi kubwa zaidi ya minara 227, huku mkoa wa Kaskazini Unguja ukiwa na idadi ndogo zaidi ya minara 25.
Katika ripoti hiyo imeainisha kuwa mikoa Mikoa ya Rukwa na Morogoro ndiyo inayoongoza kwa Ulaghai wa simu za mkononi.
Amesema mikoa mingine ambayo ulaghai unafanyika kwa kutumia simu za mikononi Mbeya ,Dar es Salaam,Arusha pamoja Pwani.
“Ulaghai umepungua kwa kiasi kikubwa katika mikoa imebaki mikoa michache ambayo bado inaendelea na ulaghai kwenye simu,”amesema Mwesigwa.
Pia Mwesigwa amesema mikoa yenye idadi ndogo ya ulaghai ni Kaskazini Unguja, Kusini Unguja na Kusini Pemba ina idadi ndogo ya majaribio.
“Ulaghai hivi sasa umepungua kwa kiasi kikubwa katika mikoa imebaki mikoa michache ambayo bado inaendelea na ulaghai kwenye simu,”alisema
Amesema kutokana na watoa huduma kufatilia na kufanyia kazi majaribio ya ulaghai yamepungua na kufikia asilimia 28.
Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi Felician Mwesigwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya robo ya tatu ya mwaka wa Fedha 2023/2023 za mwenendo wa mawasiliano nchini,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta Mhandisi Felician Mwesigwa Alakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya robo ya tatu ya mwaka wa Fedha 2023/2023 za mwenendo wa mawasiliano nchini,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau katika Mkutano wa TCRA katika utoaji wa taarifa ya mwenendo wa mawasiliano nchini.