Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amefungua maonyesho ya Tatu ya biashara ,Viwanda ,kilimo na Madini ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024 yaliyofanyika yaliyofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani mjini Babati Mkoani Manyara huku akiahidi kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kibiashara na uwekezaji ili kukuza sekta binafsi na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda ya wafanyabiashara na taasisi mbali mbali, Naibu Waziri huyo amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipambanua kuhakikisha kuwa inaweza mazingira mazuri ya uwekezaji kupitia diplomasia ya kimataifa na kuhakikisha mazingira mazuri kwa wafanyabiashara.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Biashara anayofanyika mjini Babati, Manyara.
Meneja Biashara Mati SuperBrand Gwandumi Mpoma ambao ni wadhamini wakuu, amewaomba wajasiliamali kuendelea kujitokeza kushiriki maonesho hayo ili kuweza kutangaza bidhaa zao zaidi.
Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Muhaji akitoa neno.
Makamu wa raisi wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA Taifa, Boniphace Ndengwa amesema kuwa wataendelea kudumisha ushirikiano mzuri ulipo kati ya sekta binafsi na serikali ili kuongeza wigo wa biashara na uwekezaji.
Katibu wa TCCIA Mkoa wa Manyara Mwanahamisi Rajabu ameitaka serikali itatue changamoto ya ratiba za maonyesho kufanana katika mkoa huo hali inayochangia kuzorota kwa maonyesho na baadhi ya washiriki
Kwa Upande wao wadhamini wakuu kutoka kampuni ya Mati Super Brands Limited kupitia Afisa Masoko wake Gwandumi Mpoma amesema wamekua wakidhamini kwa miaka 3 mfululizo na kuyataka makampuni mengine kujutokeza kudhamini.