Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi, walimu, wafanyakazi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zingibari iliyopo Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga Oktoba 23, 2024 ambapo vyumba vya madarasa manne na matundu nane ya vyoo vimejengwa.
…..
SERIKALI inakuja na Mpango wa kuongeza misitu ya asili kwa kila halmashauri nchini kuwa na msitu wake ikiwa moja ya njia ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira ambapo baadae itasaidia kwenye biashara ya kaboni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo Oktoba 23,2024 wilayani Kilindi mkoani Tanga wa ziara yake ya kikazi ya kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo.
Mhe. Dkt. Kijaji ameeleza kuwa lengo ni halmashauri hizo ni kuingia kwenye biashara ya Kaboni ambapo zoezi la kupandwa miti kwa pamoja litawezesha faida kuonekana haraka kuliko kupandwa na mtu mmoja mmoja.
Waziri Kijaji ameongeza mpango huo utashirikisha hasa wale ambao wana maeneo makubwa ya ardhi ambapo wanaweza kutumia ekari tano hadi kumi kwa ajili ya kupanda miti hiyo.
“Kufanikiwa kwa kupandwa miti hiyo kutasaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo mengine yanasababisha ongezeko la joto pamoja na mvua ambazo hazina mpangilio mzuri,” amesema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian amesema kumekuwepo changamoto ya wananchi kuchoma misitu hovyo na hivyo wamekuwa wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuona jinsi ya kuzuia matukio hayo.
Ameongeza kuwa mkoa huo una zaidi ya hekta laki saba za misitu ambapo ndani yake kuna mashamba matatu ya miti lakini kumekuwa na changamoto ya wananchi kuvamia na kuingiza mifugo pamoja na kuchoma mkaa, na mamlaka husika zinaendelea na udhibiti.
Amesisitiza kuwa katika mkoa huo wananchi pia wamekuwa wakijishuhurisha na kilimo cha mikokoo ambacho kinasaidia katika utunzaji wa mazingira ya bahari kwani wakati wa mmomonyoko wa udongo miti hiyo inasaidia kusitokee uharibifu kwenye maeneo ambapo mikoko ipo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na matundu nane ya vyoo katika Shule ya Sekondari Bamba Kilifi katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga Oktoba 23, 2024, mradi ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 60. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilida Burian.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikagua ubao wa kuandikia darasani katika Shule ya Sekondari Zingibari iliyopo Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga Oktoba 23, 2024 ambapo vyumba vya madarasa manne na matundu nane ya vyoo vimejengwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi, walimu, wafanyakazi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zingibari iliyopo Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga Oktoba 23, 2024 ambapo vyumba vya madarasa manne na matundu nane ya vyoo vimejengwa.
Wananchi wa Kijiji cha Mwaboza, Kata ya Moa katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo kwenye picha) ambaye yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua, kuweka mawe ya msingi na kukagua katika miradi ya maendeleo na kufanya mikutano ya kuongea na wananchi, ambapo Oktoba 23,2024 amefanya ziara Wilaya ya Mkinga na Halmashaurii ya Jiji la Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikagua miradi wakati wa ziara ya kikazi mkoani Tanga Oktoba 23, 2024.