Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha limekutana na wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo kwa lengo la kuwaelimisha kujitambua namna ya kujiepusha na vitendo vya mmomonyoko wa maadili ambavyo vinasababisha kutokea kwa matukio ya ukatili
katika jamii.
Katibu Tawala wilayani humo Bw. Joseph Mabiti wakati akiongea na wanafunzi hao leo Oktoba 25, 2024 amewataka kujiepusha na mutumizi ya dawa za kulevya, mimba za utotoni sambamba na mapenzi ya jinsia moja.
Bwana Mabiti amebainisha kuwa mitandao ya kijamii imekua mojawapo ya channzo cha kuongezeka kwa matukio hayo ya ukatili huku akiwataka wazazi na walezi kuongeza umakini kwa watoto wao kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao hiyo inayopelekea kuwepo kwa
mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Polisi Wilayani humo Mrakibu wa Polisi (SP) Beatrice Monga amesema lengo la kampeni hiyo ni kuongea na wanafunzi kabla hawajaharibiwa ambapo wanazungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza, cha tano na vyuo vikuu vyote.
SP Beatrice amefafanua kuwa Jeshi la Polisi limeamua kukutana na makundi hayo katika jamii kuwa elimu hiyo kwa sababu utandawazi umesababisha mambo yote kuwa hadharani bila ya kificho ambapo wanaenda kuwaelimisha namna bora ya kutumia mitandao hiyo kwa usahihi.
Naye Mkuu wa Dawati katika Wilaya hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Salama Ally amewaeleza wanafunzi hao umuhimu wa kuripoti matukio ya ukatili kwa haraka katika vituo vya Polisi sambamba na kwenda kutoa ushahidi mahakamani pindi watakapohitajika.
Bi. Diana Mbwambo ambaye aliwasilisja mada katika tukio hilo amewasihi wanafunzi hao kuwasikiliza wazazi na walezi mambo mbalimbali watakayowaelekeza lakini pia kujiepusha na makundi mabaya ambayo yataharibu mienendo yao ya tabia.
Itakumbukwa hivi karibuni Jeshi la Polisi lilizindua kampeni ya tuwaambie kabla ya hawajaharibiwa yenye lengo la kuongea na wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu kwa lengo la kuwaelimisha kujitambua ili kujiepusha na vitendo vya mmomonyoko maadili