Mtaalamu wa Matumizi ya Jiko Janja Daliya Charles (wa kwanza kulia) akitoa elimu ya matumizi ya Jiko Janja yayotumia Nishati ya Umeme kwa gharama nafuu kwa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini leo Oktoba 25, 2024 katika Ofisi za Shirika hilo zilizopo Magomeni, Dar es Salaam.
………
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini wamepewa elimu ya matumizi ya Jiko Janja yayotumia Nishati ya Umeme kwa gharama nafuu ukilinganisha na nishati nyingine za kupikia kama Mkaa, Kunia na Gesi.
Akizungumza leo Oktoba 25, 2024 wakati Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini wakipewa elimu ya matumizi ya Jiko janja katika Ofisi za Mkoa huo zilizopo Magomeni, jijini Dar es Salaam, Mhandisi Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni Kusini Idara ya Usambazaji, Ebenezer Fue, amesema kuwa uongozi wa Mkoa uliona kuna muhimu kwa wafanyakazi kuwa na uwelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya Nishati safi ili waweze kutumia pamoja na kuwa mabalozi wazuri wa matumizi ya nishati safi kwa wananchi.
Mhandisi Fue amesema kuwa matumizi ya Nishati safi ya umeme yana faida nyingi ikiwemo gharana nafuu tofauti na nishati nyengine.
“Mkaa wa shilingi elfu moja sawa na uniti tatu za umeme ambazo unaweza kutumia kupikia masaa zaidi ya matatu ukilinganisha na garama ya Nishati nyingine kama Mkaa ambazo kwa muda huo unaweza kutuma gharana zaidi ya hela hilo ” amesema Mhandisi Fue.
Mhandisi Fue amesema kuwa Nishati safi inaepusha na magonjwa ambayo jamii inaweza kuyapata kama ukitumia kuni au mkaa katika matumizi ya kupikia.
Kwa upande wao Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini wameushukuru uongozi wa Mkoa huo kuwawezesha kuwapatia elimu ya matumizi ya jiko janja kwani awali walikuwa hawana uwelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya jiko hilo.
Wafanyakazi wa mkoa huo wamekuwa na mwitikio mzuri wa kununua jiko janja baada ya kupata elimu na kujua faida ya matumizi Nishati safi, huku wakitoa wito kwa kwa wateja kukimbilia matumizi ya jiko janja kwani yatawasaidia kupunguza garama ya maisha.