Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tazania ,Abdul Mombokaleo katika banda la mamlaka hiyo ambao wamehudhuria kongamano mkoani Arusha .
Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tazania ,Abdul Mombokaleo katika banda la mamlaka hiyo ambao wamehudhuria kongamano mkoani Arusha .
Happy Lazaro,Arusha .
WATANZANIA wametakiwa kuzitumia kwa wingi huduma za usafiri wa anga kwani sio anasa kwani serikali inajitahidi kujenga viwanja zaidi na kuboresha miundombinu, hivyo itakuwa haina maana kama wananchi watakuwa hawajapata hamasa ya kutumia viwanja vya ndege.
Aidha wametakiwa kutumia ndege zetu na miundombinu yetu kwa faida ya ujumla kwani wanapokuwa wengi katika matumizi inawapa wao sababu ya makusudi katika kupunguza gharama kwani wakiwa wengi wanaweza kushusha gharama.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania ,Abdul Mombokaleo wakati akizungumza kwenye Kongamano la sekta ya mawasiliano na usafirishaji linaloendelea mkoani Arusha.
Amesema kuwa ,kwa ujumla maeneo ambayo wanaangalia ni ubora wa biashara zao na biashara kwa ujumla .
Aidha amewataka wananchi waelewe kuwa matumizi ya shirika la ndege sio luxury bali ni moja ya njia ambayo inaharakisha harakati za kiuchumi kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muda mfupi na ukafunga biashara yako na kurudi kwa muda mchache ,hivyo kuwataka kutumia huduma hiyo kwa wingi ili kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla .
“Maeneo ambayo tumeyapa kipaumbele ni kuangalia jinsi ya kuboresha zetu na kuboresha bei na gharama kwa ujumla katika maeneo yote .”amesema .
“Tumechukua changamoto kutoka kwa Waziri wa uchukuzi ,Prof .Makame Mbarawa kuwa tukakae chini na kuangalia namna ya kuboresha huduma hii sambamba na kuwa na huduma nzuri ambayo itawavutia watoa huduma kuja kutumia viwanja vya ndege.”amesema Mombokaleo.
Amesema kuwa,serikali inafanya jitihada kubwa sana katika kuongeza idadi ya viwanja kwa ubora wa hali ya juu na hivyo wao kuwapa changamoto au chachu ya kuweka miundombinu mizuri ya kuvutia watoa huduma mbalimbali ili kuwe na mantiki ya kutumia viwanja hivi vinavyojengwa na serikali kwa nia njema.
Akizungumzia hali ya viwanja kwa sasa amesema kuwa, kuna viwanja ambavyo vinaendelea kuboreshwa zaidi kwa maana ya kuongeza mifumo ili iwe ya kisasa na kuweza kukidhi viwango vya kimataifa kama ilivyo kwa nchi zingine.
Amefafanua kuwa ,kuna miradi inaendelea sasa hivi ya ujenzi wa viwanja vipya vya ndani na kuboresha kwani wanataka sekta ya anga pia kuwa kama sekta ya usafiri wa magari na meli kwamba kuwe na option nyingi kwa abiria .
Amesema kuwa tutaangalia eneo zima kwa maana ya abiria ,mizigo na huduma mbalimbali kwa kupitia anga japo inaonekana usafiri wa anga ni huduma ya gharama lakini malengo ya serikali ni kuifanya huduma hii iwe nyepesi na iwe na mvuto kwa wananchi.