Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 25.10.2024 imetoa elimu juu ya madhara ya kuchagua kiongozi wa Serikali za Mitaa anayejihusisha na rushwa pamoja na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya katika redio ya kijamii iitwayo Savy FM (105.3 Mhz) iliyopo Njiro jijini Arusha.
Elimu hiyo iliambatana na kuelezea mafanikio ya mwaka mmoja katika shughuli za operesheni na uelimishaji tangu kuanzishwa kwa Ofisi ya DCEA Kanda ya Kaskazini.
Pia, wasikilizaji wa redio hiyo walihamasishwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119 kwaajili ya kutoa taarifa ya wahalifu wa dawa za kulevya katika mitaa yao wanayoishi.