Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Latifa Khamis (kwanza kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Duka la Renzo Shoes Plaza Dkt. Raphael Mallaba pamoja na Mabalozi wa duka hilo Mwanamuziki wa Bongo Fleva Ambwene Yessayah (AY), Karim Mandonga akikata utepe wakati akizindua Duka la Renzo Shoes Plaza katika hafla fupi iliyofanyika leo Oktoba 26, 2024 katika ofisi za duka hilo zilizopo Kariakoo Mtaa wa Sikukuu na Tanda jijini Dar es Salaam (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Latifa Khamis (kwanza kushoto) akiwa katika Duka la Renzo Shoes Plaza akiangalia ubora wa viatu vinavyopatikana katika duka hilo.
Mabalozi wa Duka la Renzo Shoes Plaza wakishika viatu vyenye ubora wa hali ya juu.
Mkurugenzi wa Duka la Renzo Shoes Plaza Dkt. Raphael Mallaba akizungumza jambo katika hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo iliyofanyika leo Oktoba 26, 2024 katika ofisi zilizopo Kariakoo Mtaa wa Sikukuu na Tanda jijini Dar es Salaam.
…………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Latifa Khamis amezindua Duka Maalaum la kuuza viatu vya kisasa la Renzo Shoes Plaza ambalo linakwenda kutatua changamoto ya watanzania wanaopenda viatu bora na vizuri, huku akieleza kuwa Serikali inaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya biashara ili hakikisha wafanyabiashara wanafanya kazi katika mazingira rafiki.
Duka hilo la Renzo Shoes Plaza linapatikana Kariakoo Mtaa wa Sikukuu na Tanda Mti ambalo lina viatu vizuri na bora kwa gharama nafuu.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, leo Oktoba 26, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya uzinduzi wa Duka la viatu la Renzo Shoes Plaza, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bi. Latifa Khamis, amesema kuwa jukumu la TANTRADE ni kusimamia maendeleo ya biashara pamoja na kuwatangaza ili waweze kupata fursa katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Bi. Khamis amesema kuwa jukumu lao nikutoa fursa kwa wafanyabiashara mbalimbali nchini ikiwemo Renzo Shoes Plaza na wengine kujitangaza kwa kushiriki katika maonesha makubwa ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayofanyika kila mwaka.
“Tunawapongeza Renzo Shoes Plaza kwa kuja na wazo hili la kutafuta dawa kwa watu wanaopenda viatu vizuri, tunawakaribisha wafanyabiashara wengine kushirikiana na TANTRADE” amesema Bi. Khamis.
Mkurugenzi wa Renzo Shoes Plaza Dkt. Raphael Mallaba, amesema kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanauza viatu vyenye ubora wa hali ya juu na kufikia matamanio ya watanzania.
“Viatu vyetu vina ubora wa kutosha vipo vya aina mbalimbali ikiwemo viatu vya kuvaa maofisini, michezo na ubora wake ni viwango vya kimataifa” amesema Dkt. Mallaba.
Balozi wa Renzo Shoes Plaza Mwanamuziki wa Bongo Fleva Ambwene Yessayah (AY), amesema kuwa kwa sasa kuna mwamko mkubwa kwa wafanyabiashara kuendelea kupiga hatua kwa kuleta bidhaa bora kutoka mataifa mbalimbali ambazo awali zilikuwa hazipatikani nchini.
“Nitaendelea kutoa ushirikiano kwa Renzo Shoes Plaza, pia tunawakaribisha watanzania kuja kununua viatu katika duka hili kwani wana bidhaa bora” amesema AY.
Duka la Renzo Shoes Plaza linafanya kazi kwa ushirikiano na mabalozi mbalimbali akiwemo Karim Mandonga pamoja na Ay.