Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE Uchaguzi wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mtaa wa Vumilia Ukooni, Kata ya Kisarawe I| wilayani Kigay, Dar es Salaam umamalizika kwa amani leo.
Uchaguzi huo umefanyika leo Oktoba 24,2024 baada ya jana kushindwa kufanyika kutokana na vurugu zilizojitokeza na kasoro mbalimbali.
Uchaguzi huo leo hii umefanyika kwa umakini na utaratibu mzuri chini ya viongozi Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kigamboni, Viongozi wa Kata ya Kisarawe I| chini ya Katibu wa Kata hiyo Mzee Mtego.
Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi huo Rashid Ramadhan, ambaye ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kisarawe I|, alimtangaza Master John Malima kuwa mshindi, baada ya kupata kura 255, Kati ya kura 468 zilizopigwa.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Shaweji Mchonjo, aliyepata 120, wakati Thomas Mkufya ameshika nafasi ya tati kwa kupata kura 6.
Kwa upande wa Wajumbe Serikali mchanganyiko, walioshinda ni Mohamed Kitiku, aliyepata kura 247, Mohamed Mharizo kura 226 na Yusuph Lutambi aliyepata kura 191.
Wajumbe wengine walioshinda kundi la Viti Maalum ni Chiku Adinani Shakir, aliyepata kura 231 na Sarafina Mapunda, aliyepata kura 205.
Walioshindwa kwenye uchaguzi huo kwa upande wa Wajumbe na kura zao kwenye mabao ni Hillary Issa Zahoro (79), Ruben Julius’ Mihayo (45), Shaban Seleman Mwaikimba (58), Hadson Emmanuel Kihongosi (68), Hassan Juma Rumbwe (147), Halima Juma Bakari (103),
Hadija Juma Jokoro (83).
Baada ya uchaguzi huo, wanachama wa mtaa huo wametakiwa kuwa na umoja kwani hizo ni kura za maoni na vikao vitakaa kujadili na kisha kutoa mapendekezo.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unatarajiwa kufanyika nchi nzima Novemba 27 mwaka huu.