Na. Vero Ignatus, Arusha
Serikali imesema kuwa idadi ya mizigo inayopita Bandari ya Dar -es -salaam kwenda nchi nyingine imeongezeka kutoka tani Million 5.6 hadi kufikia tani million 9 ambapo kiwango cha mizigo inayohudumiwa nchi imeongeka kutoka tani Milioni 14 hadi Milioni 27
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Mwakiposa Kihenzile wakati akifunga Mkutano 17 cha tathmini ya sekta ya uchukuzi Jijini Arusha 25 oktoba 2024 ambapo amesema Sekta hiyo ni injini na mhimili muhimu katika maendeleo ya Taifa, vilevile Bandari ya Dar es salaam umekuwa miongoni mwa Bandari 6 Barani Afrika zinazohudumia makasha zaidi ya milioni 1
Kihenzike amewataka wenye viti wote wa Bodi, pamoja na Bodi zote kusimamia ipasavyo miradi yote iliyopewa fedha na kuhakikisha inakamilika ndani ya muda na kwa ubora unaostahili pia kutambua kwamba kila Taasisi inaowajibu mkubwa wa kuhakikisha Sekta kubakia kuwa mhimili wa uchumi wana nchi.
” Kama mradi inatekelezwa na haina ubora kweli kwa kufanya hivyo ninkutoitendea haki nchi yetu, Uchukuzi ni injini ya nchi katika maendeleo hivyo huwezi kuimarika. Kama hakuna mfumo uliobora na unaotegemewa na wakisasa,ndiyo maana serikali katila kuboresha miundombinu, ili kuleta ufanisi u salama wa huduma bora kwa wananchi.Alisema Kihanzile.
Aidha amelipongeza shirika la Reli nchi ni Tanzania kwa kusimamia mradi wa kisasa wa SGR ambapo kwa kusimamia mradi huo Tanzania inaunganisha nchi kama vile Congo, Burundi ambapo kitaleta tija katika biashara ya usafirishaji abiria, mizigo, hivyo kuongeza Pato la Taifa na kuchochea ukuaji wa uchumi.
“Najua zipo Changamoto, tunawataka kujipanga na kuzifanyia kazi Changamoto zote zinazooneoana katika utelelezaji wa mradi huo kutoka Dar es salaam -Morogoro ili huduma hii iweze kuwa na ubora na uhakika, na. Nahitaji kwa kweli m nahitaji pongezi.’ Alisema Kihenzile
Akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu wa Wizara ya uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema mkutano huo ulikuwa wa kikazi zaidi, katika mijadala mbalimbali waligokuwa nayo swaliweza kupata mawasilisho mengi ya kitaalam pamoja na takwimu .
“Vile vile tuliweza kuwa na Kikao cha faragha na wafadhili wetu European Union wametuambia zipo Euro billion 150 hivyo na Sisi kama nchi tutaona namna ambavyo tutaikutusaidiazipata hizo fedha Ambazo wameahidi kutusaidia”
Kahyarara amesema waliweza kuzumgumzia namna ya kubadilisha Sera kulingana na wanapoelekea ambapo Tume ya mipango inatengeneza maono ya mwaka 2025-50 ambapo wamekuwa na muda wa kuangalia kwa kina mipango na Doira kuangazia masuala (Digitalization)
“Kwa bahati nzuri tumefika mbali sana Tunawapongeza wenzetuwa Latra tuanawatengenwzea mifumo tiketi zote ziwe zinasomana na nimekua nikifuatilia hilo tayari wameshaunganisha mabasi yote na mwezi wa kumi ndiyo mwisho yawe yanasomeka katila mfumo mmoja na hayo ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia kwamba ikifika Desemba mifumo yote owe inasomana” Alisema Kahyarara
Ameainisha waliohudhurua mkutano huo wa 17 wa tathmini ya Wizara ya Uchukuzi ni pamoja na Wenye viti wa Bodi wa Taasisi zote katika wizara ya uchukuzi washiriki wa Mukutano huo wa. 17 , wakuu wa Taasisi, wadau wa maendeleo, wadau katika sekta za usafirishaji wataalamu na watendaji katika Taasisi, watendaji wa Wizara.