Askofu Dkt Benson Bagonza Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe ameitaka serikali kuziona sekta binafsi kama wadau na sio washindani.
Ameyasema hayo wakati akiongea na wazazi pamoja na wanafunzi katika mahafali ya kidato cha nne na darasa la saba kwa shule za Kaizirege na Kemebos zilizopo Bukoba Mkoani Kagera ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Aidha Askofu Bagonza ameeleza changamoto za elimu kwa sasa hususani kwa vijana wa Kitanzania na kueleza kuwa “elimu yetu inakomboa mtu na kumtenga na jamii,mara nyingi wale wanaobahatika kuipata inawapandisha mabega,inawafanya wajione ni muhimu sana na inawatenga na jamii mimi niwasihi sana elimu mnayoipata hapa iendelee kuwajaza unyenyekevu unaotakiwa ili muweze kuwatumikia watu”
“Tunahitaji elimu inayoondoa woga,inayoondoa unafiki,inayoondoa ubinafsi na kuwajaza vijana wetu kujiamini,kwa bahati mbaya kutoka na sera mbaya tulizonazo kihistoria sekta binafsi inapita katika mazingira magumu,ninaisihi serikali yetu kuziona sekita binafsi kama wadau na sio washindani”Askofu Bagonza
Pia amempongeza Mkurugenzi na muanzilishi wa Shule za Kaizirege na Kemebos Eusto Ntagalinda Kaizirege kwa jitihada alizozionyesha kuwekeza kwa upande wa elimu huku akieleza kuwa “badala ya kukusanya rasilimali zako kuwarisisha watoto wako wewe umeona bora kuwarisisha watoto wote wa Tanzania,Mzee Kaizirege angeweza kuamua kuwekeza kwa kujenga baa kila kijiji Tanzania ili watu waweze kumwagilia moyo ila akaamua fedhazote aziweke katika kituo cha elimu huu ni mchango mkubwa na kielelezo cha kuushinda ubinafsi na kielelezo cha kuonyesha uzalendo zaidi katika taifa lako” Askofu Bagonza
The post Nondo za Askofu Bagonza ,awaacha watu hoi,atoa wito kwa serikali first appeared on Millard Ayo.