Baraza la Vijana Zanzibar limewataka Wakuu wa Wilaya na Wadau wa Maendeleo kushirikiana kwa pamoja katika kuwaendeleza vijana kupitia fursa mbalimbali ili kuwainua kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Ali Haji Hassan katika ziara yake ya kujitambulisha na kukagua miradi ya Baraza Hilo kufuatia utezi aliyoupata hivi karibuni.
Amesema vijana ndio nguvu kazi ya taifa hivyo ni vyema kutumia vyema fursa wanazopatiwa ili kufikia malengo waliojiwekea.
Aidha amefahamisha kuwa ili kuwaendeleza vijana lazima kuwepo na mashirikano katika Taasisi mbalimbali ndani ya Wilaya ili waweze kufanikiwa.
Aidha amewataka vija kuwa wabunifu pamoja na kujiendeleza kielimu ili waweza kujiajiri
Amesema kuwa changammoto kubwa inayowakabili vijana ni kukosa uwezo wa kubuni miradi na kujituma hivyo Baraza linawajengea uwezo huo ili waweze kuingia katika soko la ajira.
Nae Katibu Tawala Wilaya ya Kati Hamza Ibrahim Mahamud amesema vijana ni tegemeo la taifa hivyo hivyo ni vyema kuwa na nidhamu ili kufanikiwa zaidi.
Nao vijana hao wameshukuru kwa ujio huo na kuahidi kuyafanyia KAZI yale waliyoshauriwa ili kufikia lengo.
Katika ziara hiyo Katibu Mtendaji amepata fursa ya kutembelea Kituo Cha redio jamii Kati FM Binguni na mradi wa kilimo Cha mbogamboga Muungoni.