Na. Zillipa Joseph, Katavi.
Hifadhi ya taifa ya Katavi imeadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974 .
Maadhimisho hayo yaliambatana na uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba 12 za watumishi wa hiyo kwa ufadhili wa mradi wa KAMACO.
Akisoma taarifa Mratibu wa mradi wa KAMACO bwana Msigwa amesema mradi huo wa nyumba utagharimu kiasi cha bilioni kumi na milioni mia moja na hamsini.
Pia watajenga gereji ya kisasa kwa ajili ya matengenezo ya magari, madaraja manne na vifaa vya doria .
Aidha wametenga kiasi cha shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya kuboresha mawasiliano ndani ya hifadhi.
Mkuu wa hifadhi ya Katavi bwana Abel Mtui ametaja mafanikio ya hifadhi hiyo kuwa ni pamoja na kupungua kwa vitendo vya ujangili na kuongezeka kwa idadi ya watalii wa ndani na nje.
Alisema hifadhi hiyo ni ya tano kwa ukubwa kati ya mbuga 21 zilizopo hapa na Ina wanyama wakubwa na wa kuvutia.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Sitalike mara baada ya kuzindua mradi huo Mkuu wa wilaya ya Tanganyika bwana Onesmo Buswelu ameitaka Hifadhi ya Katavi katika kuadhimisha miaka hamsini kuendelea kudumisha ujirani mwema na vijiji vinavyopakana na hifadhi.
Hata hivyo hifadhi hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA imejenga bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Sitalike kwa gharama ya shilingi milioni 192