Waziri wa Uvuvi na mifugo,Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano huo mkoani Arusha
Happy Lazaro,Arusha.
SERIKALI imeziagiza Taasisi za utafiti wa Samaki za Tanzania bara,(TAFIRI ) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (ZAFIRI )kuungana pamoja kufanya utafiti wa kiasi kilichopo cha Samaki katika ukanda wa bahari.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Uvuvi na mifugo,Abdallah Ulega,alipokuwa akifungua kongamano la 3 la watafiti wa Samaki kinachofanyika Ukumbi wa Kituo cha mikutano ya kimataifa AICC Jijini Arusha.
Amesema Taasisi hizo ziungane kufanya utafiti Ili kuwezesha nchi kuwa na uhakika wa taarifa za kutumia Ili kualika wawekezaji.
Amesisitiza pia wafanye utafiti ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa Ili kupata kiwango cha uhakika Cha Samaki kilichopo.
Amezitaja taasisi hizo kuanza hatua za kufanya utafiti wa kupandikiza Samaki kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere .
Kuhusu Vizimba,Waziri,amesema kuwa Vizimba vya uzalishaji wa Samaki katika ziwa Viktoria vimeleta mafanikio makubwa na msisiko kwa Wananchi ikiwemo upatijanaji wa chakula cha my c. Samaki na mbegu bora za Samaki.
Amesema kabla ya hatua zingine kutekelezeka kwanza tafiti za Kisayansi zirangulie ikiwemo utafiti wa Vizimba na matokeo yake watafiti watangulie.
Amewataka watafiti wafanye utafiti ziwa Victoria waonyeshe maeneo ya kuweka Vizimba lazima ziwepo ramani ili kuonyesha wapi Vizimba vya kufungua Samaki viwekwe kuondoa migogoro na watumiaji wengine wa ziwa hilo .
Amesema lengo la ramani kuondoa usumbufu na watumiaji wengine wa ziwa hilo na kuepukana na uharibifu wa mazingira na kabla hayo hayajajitokeza lazima watafiti watangulie waonyeshe maeneo hayo.
Naibu Katibu mkuu anaeshughulikua Uvuvi,Dokta Edwin Mhede amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuhakikisha kuna kuwa na ulinzi wa rasilimali na mazao ya Uvuvi.
Amesema Wizara inatekeleza lengo la 14 la Umoja wa mataifa la kuimarisha uhai wa viumbe vya baharini.
Amesema kuwa kongamano hilo linashirikisha Wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kimataifa za utafiti wa samaki kutoka nchi 15 Ulimwenguni ,Vyuo vikuu na. hiyo ni fursa kwa Wizara kuzungumzwa na wadau wa Sekta binafsi.
Amesema tafiti hizo ni muhimu sana mwezi Mei mwaka huu Serikali ilibidi kupumzisha shughuli za Uvuvi ziwa Tanga yika Kwa kipindi cha miezi mitatu na sasa Samaki wameongezeka sana.
Mkurugenzi mkuu waTaasisi ya utafiti wa samaki TAFIRI. Ismail Kimerei,amesema kuwa Mkutano huo watatu wa Sayansi na Uvuvi wa Uchumi wa bluu endelevu.
Amesema watawasilisha matokeo ya utafiti katika maeneo Tisa ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ,Teknolojia ya Ufugaji wa viumbe maji ,Usimamizi wa rasilimali katika bahari
Amesema katika kipindi cha miaka miwili wamefanya tathimini ya mtawanyiko wa Samaki katika bahari maziwa na mito.
Amesema Serikali imeweka mpango mkakati wa kuondoa 60% ya upitevu wa Samaki ifikapo mwaka2030.
Amesema uukosefu wa takwimu sahihi ni tatizo linalozitesa nchi nyingi duniani hivyo wanatengeneza mfumo ambapo Wananchi wenyewe kwenye mialo wanatoa taarifa za Samaki kwa kupiga picha.
Ameongeza kuwa teknolojia inawezesha kutambua maeneo yenye Samaki.na hivyo kumwezesha mvuvi kuvuka eneo lenye Samaki wengi.