Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amesema Serikali imepata mafanikio mazuri kwa kuongeza idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi kutoka 88% Mwaka 2022 hadi kufikia 98% Mwaka 2024.
Dkt Yonazi amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa wanaotekeleza Afua za Vijana Balehe nchini, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya jamii Jinsia Wanawake na Makundi Makundi Maalumu unaofanyika kuanzia 31 Oktoba hadi Novemba 2024 Mkoani Dodoma.
Ameeleza mafanikio hayo yanatokana na juhudi kubwa zinazofanywa na wadau kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan na katika kuhakikisha vijana wanaendelea kulindwa na kuwezeshwa kwa ajili ya faida na maendeleo ya nchi yetu.
Kwa kupitia kauli mbiu yetu ya “Utatuzi wa Changamoto za Vijana balehe kwa taifa imara, inatuhimiza kuhakikisha vijana wetu wanakuwa na ustawi mzuri kwa ajili ya uimara wa taifa letu,” amesema Dkt, Yonazi.
Aidha mafanikio mengine yaliyoletwa Afua za Vijana Balehe nchini kwa mujibu wa taarifa ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiri vya Tanzania Mwaka 2022 inaonesha kupungua kwa mimba za utotoni kutoka 27% kwa Mwaka 2015-2016 hadi 22 Mwaka 2022.
Ameeleza, “kupungua kwa vitendo vya ukeketaji 2015-2016 kutoka 10% hadi kufikia 8% kwa Mwaka 2022 ikienda sambamba na kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 45 kutoka 40% Mwaka 2015-2016 hadi kufikia 27% Mwaka 2020-2022”.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Bw, Amon Mpanju amesema uwekezaji wa afya katika maswala ya kitaifa na maendeleo ya vijana balehe umelenga katika kufanya tathimini juu ya Afua mbalimbali zinazotekelezwa na wadau kupitia katika sekretarieti za Mikoa na Halmashauri mbalimbali hapa nchini.
Lengo likiwa ni kuanisha changamoto nakupata ufumbuzi wa namna bora ya kuboresha uwekezaji zaidi katika maswala ya afya na maendeleo ya vijana ambayo imebebwa na nguzi sita zinazopaswa kutekelezwa, alifafanua.
“Kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa vijana balehe, ikiwemo kuzuia ukatili kwa vijana ukihusisha ukatili wa kimwili. Ukatili wa kingono, ukatili wa kihisia,” alisema Naibu Katibu Mkuu Mpanju
Aidha mikakati ya serikali inalenga katika kuzuia mimba za utotoni kwa vijana balehe kwa kuhakikisha wanapata elimu sahihi na kuendelea kuimarisha hali ya lishe kwa vijana balehe ili kutengeneza taifa imara la kesho.
Pia kuendelea kuhakikisha vijana wanaendelea kubali shuleni ili kuendeleza ndoto zao za elimu kama nyenzo kubwa ya ukombozi ili kujenga tija kwa Taifa.
Naibu Mpanju amesema, “serikali itaendelea kuhakikisha vijana wanapata mafunzo ya kuongeza ujuzi zinazowasaidia kujijengea uwezo wa kujitegemea kwa misingi ya kuajiriwa na kujiajiri.”