Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akiwa amepozi kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa Jeshi la akiba kwenye mahafali yaliyofanyika Kata ya Manerumango Mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba ambayo yamefanyika leo terehe 1,Novemba ,2024 Kata ya Manerumango Mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Petro Magoti ambaye alikua mgeni rasmi kwenye mahafali ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba yaliyofanyika leo tarehe 1,Novemba 2024 Manerumango Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amewaasa wahitimu wa mafunzo wa Jeshi la akiba kutorubuniwa na wanasiasa mara baada ya kupata mafunzo hayo.
“Msijingize kwenye makundi ya wanasiasa ambao hutumia mbinu za kuwarubuni kwa sababu wanafahamu mmepewa mafunzo ya ulinzi na usalama wa raia nawasisitiza nendeni mkawe makini na kuzingatia kiapo chenu” amesema DC Magoti.
Nawaahidi kuwa nitawapa kazi hivyo hamtokuwa mkizagaa mitaani Kisarawe ina kazi nyingi za kufanya hivyo nanyi mnapaswa mkawe wazalendo.
DC Magoti amesema hayo leo Novemba Mosi alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo ya jeshi la akiba yamefanyika kwa muda wa wiki 16 ya kundi la 23 mwaka 2024 ambayo yamehusisha vijana 119.
Akisoma risala kwa niaba ya wenzake mhitimu wamafunzo hayo Nasma Hamisi Chingwile amesema kuwa wanaomba ziwekwe sheria kali kwa taasisi mbalimbali ambazo hutoa ajira za ulinzi kwa watu ambao hawajapitia mafunzo na mbinu walizopewa wao.
“Tunaomba serikali itupe kipaumbele pindi ajira zinapotokea kwenye Majeshi yetu ikiwa pamoja na Jeshi la Polisi Idara ya Uhamiaji na JKT “amesema Chingwile.
Wakati huohuo ameongeza kwa kusema kuwa wakufunzi wao wawezeshwe kwa kuboreshewa maslahi mazuri ili waweze kuwafundisha kwa ari zaidi vijana hao wa jeshi la akiba.
Awali akizungumza kuhusu changamoto wanaozipitia kwenye mchakato wa mafunzo Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Kisarawe Meja Silvery Mabubu amemweleza DC Magoti kuwa wanakabiliwa na ukata wa fedha za kujikimu kwa vijana wawapo mafunzoni hali ambayo husababisha wakatishe mafunzo na kwenda kufanya vibarua ili wapate fedha za kununua sare zao.
“Mheshimiwa vijana wetu wanakumbana na changamoto ya mavazi jambo linalopelekea baadhi yao kukatisha mafunzo na kwenda kufanya vibarua ili waweze kupata fedha za kujikimu kwa manunuzi ya sare zao hivyo tunaiomba Halmashauri ya Kisarawe ilibebe hili jambo hili ambalo la muhimu na lizalendo ” amesema Meja Mabubu.