Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti ya Manunuzi ya Umma (PPRA ) Dennis Simba akizungumza na Wahariri Vyombi vya Habari katika Mkutano wa kueleza mafanikio kwa Mfuko huo kwa kipindi cha Miaka mitatu cha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kanda ya Pwani wa PPRA Vicky Mollel akizungumza kuhusiana na mfumo wa Nest kwa wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akizungumza kuhusiana na umhinu wa upashanaji wa hababri kwa PPRA katika kuwafikishia wananchi habari jijini Dar es Salaam.
*Zaidi ya sh.bilioni 14 zimekuolewa kwenye manunuzi ya mwaka wa Fedha 2023/2024
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imesema kuwa asilimia 70 bajeti ya serikali inatumika katika manunuzi ya umma.
Bajeti hiyo bunge hadi inapita wabunge wanakaa kwa muda miezi minne hivyo kunahitajika udhibiti huo wa manunuzi katika kuipusha Serikali katika matumizi yatakayoitia hasara.
Mamlaka hiyo imeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 14.94 kupitia ukaguzi na shilingi trilioni 2.7 kupitia ufuatiliaji katika mwaka wa fedha 2023/2024 imeokoa
Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Bw. Dennis Simba wakati wa kikao kazi na Wahariri vyombo vya habari na Waandishi Waandishi wa habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).
Simba amesema katika wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) Nest hadi kufika Oktoba 31, 2024 Taasisi Nunuzi 21,851 zimesajili na kutumia mfumo huo.
Pia,bajeti ya ununuzi ya zaidi ya shilingi trilioni 38.6 imewekwa kwenye Mfumo wa NeST, kama fursa ya wazi kwa ajili ya wazabuni.
Simba amesema wazabuni zaidi ya 28,590 wamejisajili kwenye Mfumo wa NeST huku mikataba ya zabuni 62,267 yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 10.2 imetolewa kwa wazabuni kupitia Mfumo wa NeST.
“Ununuzi wa umma ni shughuli muhimu ya kiuchumi inayohusisha sehemu kubwa ya Pato la Taifa (GDP) takribani asilimia 70 ya bajeti ya Serikali na taasisi zake hutumika kwenye ununuzi wa umma”amesema
Amesema katika ununuzi wa umma umekuwa sheria yake ikibadilishwa ili kudhibiti ununuzi wa umma pamoja na kwenda na wakati uliopo ambapo sharia inayosimamia ni Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410.
Amesema, sheria hiyo imeunda Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo.
“Chini ya sheria hii zimeundwa Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2024 na Miongozo kwa ajili ya kuweka taratibu za ununuzi wa umma. Kanuni mpya za Ununuzi wa Umma zimekwishakamilika.”
Simba ameongeza kuwa, pia mamlaka hiyo imewezesha ushiriki wa makundi maalum katika ununuzi wa umma na kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa wananchi kwa kuanzisha kanda sita katika mikoa ya Mwanza, Dar es Saalam, Arusha, Mbeya,Tabora na Mtwara.
“Na tumekamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya PPRA na kuhamia rasmi tangu mwezi Machi 2024 na hivyo kuokoa pesa ambayo ingetolewa kama kodi ya pango.
Amesema, katika kuwaongezea nguvu wazabuni wa ndani, sheria mpya ya ununuzi wa umma imeweka fursa ya wazabuni wa ndani kushirikiana na wazabuni wa nje (partnership), na katika ushiriki huo, kampuni ya ndani ndiyo itakayokuwa kampuni kiongozi na fedha zitalipwa kwa kampuni hiyo ya ndani.
“Zabuni zenye thamani isiyozidi shilingi bilioni 50 zimetengwa kwa ajili ya wazabuni wa ndani ya nchipekee.Mfumo wa NeST unaisaidia PPRA katika kulisimamia hilo kwa ufanisi zaidi.”
Amesema,Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura 410, inazitaka taasisi za Serikali kutenga asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi kwa ajili ya makundi maalum, ambayo ni vijana, wanawake, wazee na watu wenyeulemavu ambapo Mfumo wa NeST kama nyenzo, umesaidia utekelezaji wake.
Simba amesema tangu mfumo wa NeST ulipoanza kutumika Julai 1, 2023 hadi Oktoba 8, 2024, jumla ya vikundi 210 (makundi maalum( vilifanikiwa kupata tuzo za zabuni zenye jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 9.855.
“Katika mwaka wa fedha uliopita, yaani tangu Julai 1, 2023 hadi Juni 30,2024 kwa ujumla, vikundi 85 vya vijana vilipata zabuni zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu na milioni mia tisa.”
Simba amesema,katika makundi mengine, tangu Julai 1, 2023 hadi Juni 30,2024 vikundi 84 vya wanawake vilipata zabuni zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni Nne na vikundi viwili vya wazee vilipata zabuni zenye thamani ya shilingi milioni 74.
Baadhi ya wahariri katika mkutano wa PPRA jijini Dar es Salaam.