Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametangaza siku ya Jumanne, Novemba 5, kumtimua Yoav Gallant kwenye wadhifa wa Waziri wa Ulinzi.
Nafasi yake inachukuliwa na Israel Katz aliyeshika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje. “Imani” katika Yoav Gallant “ilipungua” wakati wa vita huko Gaza, anasema Benjamin Netanyahu. Gideon Saar ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumanne jioni alimfukuza kazi Waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant, ambaye uhusiano wake ulikuwa na mvutano wakati wa vita huko Gaza, na kumteua badala yake mkuu wa sasa wa diplomasia ya Israel Katz. Wizara ya Mambo ya Nje imekabidhiwa Gideon Sarr, ambaye hadi wakati huo alikuwa waziri asiye na wizara maalum.
“Katikati ya vita, uaminifu unahitajika zaidi kuliko hapo awali kati ya Waziri Mkuu na Waziri wake wa Ulinzi,” lakini “katika miezi ya hivi karibuni, uaminifu huu ulipotea,” Bw. Netanyahu amesema katika barua aliyomuandikia Bw. Gallant, na kuongeza kuwa “amechagua kumteua Waziri Israel Katz kuchukua nafasi yake.”
“Tofauti kubwa ziliibuka kati ya Bw. Gallant na mimi mwenyewe katika uendeshaji wa kampeni (ya kijeshi), ikiambatana na kauli na vitendo vinavyopingana na maamuzi ya serikali na baraza la mawaziri,” ameongeza.
Yoav Gallant alijibu kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba “usalama wa Israeli umekuwa na utabaki kuwa dhamira ya maisha [yake].”
Mkuu wa sasa wa diplomasia, Israel Katz, “tayari ameonyesha uwezo wake na mchango wake kwa usalama wa taifa,” ameandika Benjamin Netanyahu kuelezea chaguo lake.
The post Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amfuta kazi waziri wake wa ulinzi first appeared on Millard Ayo.