NA MWANDISHI WETU
Alisema kwa kufanya hivyo itasaidia kuleta maana halisi ya kaulimbiu inayesema (Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa uchumi endelevu) akieleza kwamba ujuzi na bunifu ni nyezo muhimu katika taifa lolote linalohitaji maendeleo.
Wito huo ameutoa jana Novemba 7, 2024 wakati akihutubia katika mahafali ya 14 ya Chuo cha VETA Pwani, ambapo alikuwa mgeni rasmi.
“Nitumie nafasi hii pia kutoa wito kwa taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Serikali kwa kusaidia ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye uhitaji hasa wale wanaotoka kwenye mazingira magumu,” alisema Asma.
Aidha katika Mahafali hayo, Asma aliahidi kutoa mifuko 100 ya Saruji kwaajili ya kwenda kusaidia kuboresha miundombinu ya kijifunzia katika chuo hicho.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Pwani Clara Kibodya ameziomba asasi zisizo za kiserikali na wadau mbalimbali kuendelea kufadhili vijana walio katika mazingira magumu kwa kutambua mahitaji yao na kisha kuwapeleka VETA ili kupatiwa mafunzo elimu ya ujasiriamali.
Alisema mafunzo hayo yatawatengenezea fursa za kujiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kwamba hiyo itapunguza wimbi la vijana wasio na ajira.
“Mafunzo ya VETA huendeshwa kwa mfumo wa ufundi mahiri ambao unalenga na kuzingatia ujuzi unaoendana na soko la ajira. Muundo mzima wa mafunzo humpatia mwanafunzi mazoezi mengi ya vitendo, elimu ya nadharia na tabia, sambamba na mafunzo viwandani, hivyo yatasaidia vijana wetu kutumia ujuzi watakaupata kujitengenezea kipato,” alisema Clara.