Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 7,2024, kuhusiana na Kongamano la Uwekezaji litakalofanyika nchini Saudia Arabia katika mji wa Riyadh.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Rafael Maganga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 07,2024 kuhusiana na Kongamano litakalofanyika nchini Saudia Arabia katika mji wa Riyadh Desemba 17-20, 2024. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri.
Msimamizi wa Mashariki ya kati kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Juma Nzima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 07,2024 kuhusiana na Kongamano litakalofanyika nchini Saudia Arabia katika mji wa Riyadh Desemba 17-20, 2024.
Wafanyabiashara zaidi ya 100 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kushiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji nchini Saudi Arabia, lilioandaliwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF).
KATIKA kutambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa Kushirikiana na taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia wameandaa kongamao la siku tatu Uwekezaji kati ya Tanzania na Saudi Arabia litakalofanyika kati ya Desemba 18 -20, 2024 nchini Saudia Arabia katika mji mkuu wa Riyadh.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 07, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri ametaja sababu za kwanini kongamano hilo lifanyike Saudia Arabia, ameeleza kuwa nchi ambazo zinauchumi mkubwa duniani na ni wanachama wa nchi za G20.
Pia ameeleza kuwa ni nchi ambayo ina rasilimali ya mafuta pamoja na gesi.
Pia Teri ameeleza takwimu za uwekezaji wa Wasaudia Arabia nchini Tanzania hadi kufikia Oktoba 2024. Amesema kuwa Saudia Arabia imewekeza zaidi ya dola milioni 63 katika uchumi wa Tanzania na kutengeneza ajira 1126 kwenye miradi zaidi ya 17 ambapo wamewekeza katika kilimo, Utalii, huduma, Uchukuzi na ujenzi.
Kwa Upande wa Msimamizi wa Mashariki ya Kati kutoka TIC, Jumza Nzima ameeleza kuwa Msafara utaanza safari Desemba 17 na 18 Kongamano litaanza ambapo kutakuwa na mawasilisho mbalimbali kutoka kwa waalikwa, Desemba 19 kutakuwa na mikutano na majadiliano mbalimbali yatakuwa yanaongozwa na sekta husika ambazo ni Kilimo, ujenzi, uchukuzi, Utalii, sekta ya madini, sekta ya usafiri na usafirishaji na sekta ya mafuta na gesi.
Na siku ya tatu katika kongamano hilo, Nzima ameeleza kuwa Desemba 20 inakuwa ni siku ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yatakuwa yameainishwa katika sekta hizo sita. Na Desema 21 safari ya msafari kurudi itaanza.
Licha ya ratiba hiyo, Nzima amesema kuwa katika kongamano hilo wadau kutoka sekta mbalimbali wataweza kuonesha na kuelezea bidhaa zao ndani ya ukumbi wa kongamano hilo.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Rafael Maganga amesema kuwa wafanyabiashara zaidi ya 100 watahudhulia kongamano hilo kwani kumekuwa na mafanikio makubwa ya ziara hizo kwa watanzania wanaoshiriki safari mbalimbali za nje ya nchi.
Pia ameeleza malengo ya safari ya kongamano la Saudia Arabia kuwa ni kutafuta masoko, Kuonesha fursa za uwekezaji, Kukuza ubia kati ya kampuni za Tanzania na Saud Arabia, kubadilishana uzoefu kati ya kampuni za Tanzania na za Saudia Arabia pia kujifunza teknolojia pamoja na kukuza ajira kwa waatanzania wanatafuta ajira ndani ya Tanzania na Saud Arabia.
Aidha wafanyabiashara na wawekezaji wamehamasishwa kujiandikisha mapema kuweza kushiriki katika kongamano hilo kupitia mitandao ya kijamii pamoja na website za TIC @invest_in_tanzania , ZIPA @zipazanzibar pamoja na TPSF @tpsf_tanzania.