Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Christian Nyakizee akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Christian Nyakizee.
…….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni imefanikiwa kufatilia miradi sita yenye thamani ya Sh 15,982,221,355.9 ambayo inaendelea na utekelezaji pamoja na kuwajengea uwezo Maafisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni pamoja na Askari Polisi Dawati la Jinsia na Watoto kwa ajili ya kutatua kero ya ukatili wa kingono kwa watoto na jamii kwa ujumla unaochangiwa na vitendo vya rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu, kuanzia Julai 2024 hadi Septemba 2024, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni Bw. Christian Nyakizee, amesema kuwa katika kufatilia miradi wamebaini mapungufu machache ambayo wahusika wameshauriwa kurekebisha, huku akisisitiza kuwa wanaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Bw. Nyakizee amesema kuwa katika kipindi hicho wametoa mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jahmiimkutoka kata zote za Wilaya ya Kinondoni ambapo walisisitiza umuhimu wa kutimiza wajibu wao kwa kufuata Sheria, you nKanuni, Taratibu na Miongozo ili ku TVleta tija katika utendaji kazi na kufikia malengo.
“Pia Askari Polisi Dawati la Jinsia na Watoto walishiriki mafunzo ili kushughulikia kero za Dawati ikiwemo vitendo vya rushwa na kurahisisha utendaji kazi wa Dawati ili kufikia lengo la serikali ambalo ni Ustawi wa wananchi” amesema Bw. Nyakizee.
Amefafanua kuwa jumla ya Askari Polisi 37 kutoka kwenye madawati 14 wa Kinondoni ambayo ni Oysterbay, Kijitonyama, Chuo Kikuu cha DSM, Magomeni, Urafiki, Mburahati, Gogoni, Magufuli Bus Terminal, Mavurunza, Kawe, Mbweni, Mabwepande, Goba na Madale waliofanikiwa kushiriki mafanzo hayo.
Amesema kuwa pia wamepokea jumla ya malalamiko 104, huku Malalamiko yaliyohusu rushwa yalikuwa 72 na yasiyohusu rushwa ni 32.
Bw. Nyakizee amesema kuwa wamefanikiwa kufungua mashauri mapya mawili (02) katika Mahakama ya Wilaya ya Ubungo, huku mashauri saba (7) yalitolewa maamuzi na Jamhuri imefanikiwa kushinda mashauri matatu (3) na mashauri 24 yanaendelea mahakamani.
“Tumejipanga kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuelimisha Wananchi wajue madhara ya rushwa na wahamasike kushirikiana na TAKUKURU kutokomeza rushwa kuanzia sasa hadi wakati na baada ya uchaguzi” amesema
Bw. Nyakizee.
TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni tu
inatoa wito kwa wananchi wote kuendelee kutoa ushirikiano na kuwasihi kuendelea kutoa taarifa zozote za rushwa kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi kwa namba ya dharura kupitia namba 113 na kufuata maelekezo au kufika katika ofisi yoyote ya TAKUKURU.