Dar es Salaam, Tanzania-12 Novemba 2024
Kampuni ya iTrust Finance imezindua rasmi Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja, mpango ambao unalenga kuwawezesha wawekezaji kuwekeza kwa pamoja katika mchanganyiko wa dhamana mbalimbali kama hisa, hati fungani, amana za benki, na dhamana nyinginezo.
Mfuko huu unafanya kazi kwa kupitia ngazi tano kuu. Kwanza, fedha hukusanywa kutoka kwa wawekezaji mbalimbali wakiwemo watu binafsi, vikundi, taasisi, na mashirika mengine. Pili, mfuko huongozwa na msimamizi mtaalamu wa uwekezaji ambaye husimamia uwekezaji ili kuhakikisha unafanyika kwenye mchanganyiko sahihi wa dhamana.
Ngazi ya tatu ni mseto wa dhamana, ambapo hisa, hati fungani za makampuni na serikali, pamoja na amana za taasisi za fedha huwekezwa ili kuongeza mapato huku ukipunguza hatari. Katika ngazi ya nne, mfuko hupata mapato kupitia dhamana zinazoshikiliwa, kama vile faida za riba na kuongezeka thamani kwa hisa. Hatua ya tano ni kugawana faida, ambapo mapato yaliyopatikana hugawanywa kwa wawekezaji kwa uwiano sawa, hivyo kuongeza thamani ya vipande vya mfuko.
Kuwekeza katika mfuko wa iTrust Finance kuna faida kadhaa. Kwanza, mseto wa dhamana unasaidia kupunguza hatari ya hasara na kuongeza uwezekano wa mapato. Pili, mfuko huu unawapa wawekezaji urahisi wa kuchangia kulingana na malengo yao ya kifedha.
Aidha, mfuko huu una ukwasi kwa wawekezaji, ambao wanaweza kutoa sehemu au jumla ya uwekezaji wao ndani ya siku tatu za kazi. Pia, mfuko unatoa fursa pana za uwekezaji ambazo zinaweza kuwa ngumu kwa mtu mmoja mmoja kuzifikia. Vilevile, mfuko unasimamiwa na meneja mtaalamu ambaye anafanya maamuzi kwa niaba ya wawekezaji, huku udhibiti na uwazi ukihakikishwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ili kulinda maslahi ya wawekezaji.
iTrust Finance inatoa mifuko mbalimbali ya uwekezaji wa pamoja, ikiwemo:
iSave: Mfuko kwa malengo ya akiba.
iCash: Mfuko kwa malengo ya kupata fedha haraka.
Imaan: Mfuko unaolenga malengo ya muda mrefu.
iIncome: Mfuko ambao hutoa gawio la mara kwa mara kwa wawekezaji.
iGrowth: Mfuko unaolenga kukuza mtaji wa mwekezaji.
Ili kuwekeza katika mifuko ya iTrust Finance, tembelea tovuti yao kupitia kiungo https://linktr.ee/itrust_finance_limited au skani QR code iliyoambatanishwa.