Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umeme Plus Ltd , Roman Shayo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kampeni hiyo.
……..
Happy Lazaro, Arusha .
Kampuni ya wauzaji wa vifaa Bora na vya kisasa vya umeme na taa ya Umeme Plus Ltd imezindua rasmi kampeni mpya ya msimu wa sikukuu kwa ushirikiano wa watengeneza maudhui kwenye mitandao ya kijamii .
Aidha vifaa hivyo vya umeme vya kisasa zikiwemo taa za urembo vimekuwa vikiagizwa nje ya nchi na kuuzwa kwa bei ya jumla kwa kuzingatia mahitaji ya wateja .
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusu kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umeme Plus Ltd , Roman Shayo amesema kuwa wamefikia hatua ya kuandaa kampeni hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kurudisha kile wanachopata kwa jamii.
Amesema kuwa ,kampuni hiyo ilianza rami mwaka 2020 hivyo imetimiza miaka 4 sasa hivi na wameona ni vizuri kurejesha kwa jamii kile walichopata kwa wale wote waliokuwa wakiwasapoti wakiwemo wazazi,shule mbalimbali,makanisa na wadau mbalimbali .
“Tungependa wateja wetu wafahamu kuwa Sisi ni mabingwa katika uuzaji wa vifaa vya umeme na taa nzuri za kisasa kwa kualika watu wenye ushawishi kushiriki uzoefu wao na bidhaa za duka kwenye mitandao ya kijamii “amesema Shayo.
Aidha amesema kuwa, wanatarajia kuanzisha mashindano ya pooltable yatakayowakutanisha vipaji vya ndani ya Arusha na nje ya Arusha na kuonyesha ujuzi wao chini ya taa za kisasa zitakazofungwa na kampuni hiyo ya Umeme Plus kama mdhamini wa shindano hilo ambapo tukio hilo halitawaburudisha tu jamii bali pia litaonyesha nguvu ya kubadilisha ya Suluhu za taa za kisasa.
Aidha amesema kuwa, kampuni hiyo imelenga kuwezesha vijana kwa kufanya (youth badass Ghettos) ambapo kampuni hiyo itafanya challenge ya vijana na watu binafsi wenye nyumba nzuri kushiriki challenge inayoitwa “Youth Badass Ghettos”ikialika vijana kuonyesha video za nyumba zao kwenye mitandao ya kijamii na kuomba comments kwa wafuasi wao,ambapo mshindi wa challenge hiyo atapata huduma ya kuboreshewa taa za nyumbani kwake kutoka kampuni hiyo.
“Kwa viongozi wa dini kampeni hii itaenda pia kwa viongozi wetu wa dini wachungaji,mashehe kushiriki katika challenge hii kupitia ukurasa wa Instagram wa kampuni hiyo ,kwa kutupa sababu za kwa nini wanastahili kupata taa zetu kama sehemu ya kampeni yetu ya mwisho wa mwaka “amesema Shayo.
Hata hivyo amesema kuwa vituo vya watoto yatima vitazingatiwa kwa mpango huu,kuonyesha kujitolea kwetu lakini na wao wanapaswa kutupa sababu kwa nini wao kampeni hii inafaa kuwapitia na wao pia .
Aidha kampuni hiyo imejitolea kutoa vifaa vya umeme na Suluhu za taa za ubora wa juu,kwa kuzingatia ubunifu wa hali ya juu na kuridhika kwa wateja , na wanalenga kuboresha maisha ya wateja kupitia teknolojia ya kisasa na huduma bora.
Kwa upande wa mabalozi wa kampuni hiyo ya Umeme Plus Ltd,Mama Nairo na Gerald Jackson wamesema kuwa,ni vizuri wananchi wa Arusha wakajitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na kampuni hiyo ili waweze kujishindia vifaa bora na vya kisasa .