Na Mwandishi Wetu.
MADAKTARI Bingwa wa Taasisi ya Saratani ya OCEAN ROAD wameshirikiana na uongozi wa Mkoa wa Simiyu akiwemo Katibu Tawala Prisca Kayombo, katika utoaji huduma za uchunguzi wa saratani kwa siku saba mkoani humo.
Madaktari hao wakiongozwa na Meneja Huduma za Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma Dkt.Maguha Stephano,amesema huduma za uchunguzi na ugunduzi wa Saratani kwa wananchi wa Simiyu ni muhimu.
Amesema huduma hizo za kibingwa zinazotambulika kama Dkt Samia Suluhu Hassan Uchunguzi na Matibabu ya Saratani ni mpango wa serikali katika kuhakikisha wananchi hususani wa pembezoni wanafikiwa na huduma za awali za matibabu.
“Huduma hizi zinatolewa bila malipo na tunatarajia kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa wa pembezoni, lengo la serikali ni kuhakikisha watu wanafanyiwa uchunguzi mapema na wale wanaobainika kuwa na Saratani wanapatiwa huduma kwa wakati,”amesema.